WAZIRI MKUU: TUTAENDELEA KUWASHIRIKISHA WAVUVI NA WAFUGAJI KWENYE MIPANGO YA MAENDELEO

 

Waziri Mkuu Kassim Majakiwa amesema Serikali  inaendelea kujikita katika kuhakikisha inaimarisha na kuwashirikisha wavuvi na wafugaji katika mipango ya maendeleo.

Amesema hayo leo Juni 03, 2024 alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa soko la samaki la kisasa la Chato Beach, Chato mkoani Geita.

Amesema kuwa Mradi huo unaotoa fursa kwa yeyote aliyeanza na anayetaka kujikita kwenye sekta ya uvuvi kunufaika na kujiingizia kipato. “Kitendo cha Serikali kuleta soko hili hapa ni kuhakikisha wanasogeza fursa kwa wavuvi  wa eneo hili, soko hilo ni lenu, imarisheni uchumi wenu kupitia soko hili”.

Ameongeza soko hilo litakuwa na uwezo wa kukausha hadi tani 10 za dagaa kwa siku kwa kuwa kutawekwa mtambo wa kukausha samaki. “Tutaweka mafriji makubwa mawili ya kutunzia samaki, pamoja na chumba maalum cha kuzalisha barafu”

Ujenzi wa soko hilo ambalo umefikia asilimia 90 utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.75 na utasaidia kupunguza upotevu wa samaki hasa dagaa baada ya kuvunwa, kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi, kutoa ajira zipatazo 1473 kwa wavuvi, wafanyabiashara na wachuuzi na kuimarisha ukusanyaji wa takwimu za uvuvi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post