TGNP YAENDELEA NA ZOEZI LA URAGHBISHI KASULU

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughuikia Idadi ya Watu (UNFPA), wameendesha zoezi la utafiti shirikishi  wa kijamii (PAR) katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu kuiwezesha jamii kuibua, kuchambua na kuweka mikakati ya kutokomeza vitendo vya Ukatili wa Kijinsia katika jamii. 


Uraghibishi huu unafanyika katika kata za Murusi na Kumsenga zilizopo Halmashairi ya Mji wa Kasulu, Mkoani Kigoma. Zoezi hili limehusisha wananchi kutoka katika vikundi vya wanawake  na wanaume zaidi ya 30, na washiriki wapatao 50.

 Uraghibishi huu unatumia mbinu shirikishi ya Uibuaji, Uchambuzi na kuweka mipango ya Utekelezaji (U-3) katika kubaini sababu za tatizo la Ukatili wa kijinsia na kuweka mikakakti ya kutokomeza vitendo hivyo katika jamii.


Hii ni sehemu ya Utekelezaji  wa Mradi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa, chini ya UNFPA, wilayani Kasulu, unaolenga pia kutokomeza Ukatili wa Kijinsia kwa wanawake na watoto ili kuwawezesha kushiriki kwenye shughuli za kimaendeleo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post