SERIKALI MARA YAJA NA MKAKATI WA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO


Katibu Tawala Mkoa wa Mara Gerald Kusaya akipokea vifaa hivyo hivi karibuni

Na Frankius Cleophace Bunda.


Serikali mkoani Mara imeweka mikakati ya kupunguza vifo vya watoto wachanga pamoja na akina Mama ili kuhakikisha watoto wanakuwa salama wakati wa kijifungua na baada ya kujifungua.


Akiongea katika kikao cha robo ya mwaka mganga mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt Zabron Masatu alisema kuwa kwa takwimu za Januri mpaka Machi mwaka 2024 zinaonesha kuwa kumekuwepo na vifo vya watoto 172 wakati mama akijifungua na wengine baada ya kujifungua.


“Licha ya vifo vya watoto wachanga pia kuna vifo vya akina mama 15 kwa Mwezi Januari Machi hivyo kupitia kikao hiki tunaendelea kutoa msisitizo kwa wataalamu ili kupunguza vifo hivyo”, alisema Dkt. Masatu.


Masatu aliongeza kuwa baadhi ya vifo watoto hutokea tumboni kutokana na wazazi kuchelewa kufika hospitali mapema ambapo amesisitiza sasa jamii kuwa na mazoea ya kufikisha wajawazito mapema kwenye vituo vya Afya ili kupatiwa huduma mapema kwa ajili ya kuzuia vifo ambavyo siyo vya lazima.Masatu alisema kuwa kupitia kikao hicho sasa wameweka mikakati ya pamoja ili kuzuia vifo hivyo nakusisitza kuwa serikali imeboesha sekta ya Afya hivyo hawatarajii tena kuona takwimu za vifo hizo zikipanda.Katika kupambana na tatizo hilo,shirika lisilo la kiserikali la Jhpiego kupitia mradi wake wa USAID Afya Yangu-Mama na Mtoto limetoa vifaa vya afya kukabiliana na vifo vya mama na motto ikiwa na lengo la kupunguza vifo vya Mamana Mtoto Mkoani Mara.


Vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 38 vimekabidhiwa ofisi ya mkuu wa mkoa ambavyo vitapelekwa kwenye wilaya za mkoa wa Mara.


Akikabidhi vifaa hivyo mratibu wa mkoa wa mradi huo Erick Bakuza alisema kuwa vifaa vitakwenda kusaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto.


“Leo tumeona Takwimu za vifo vya mama na mtoto mkoa wa Mara sasa lengo letu nikuhakikisha hizo takwimu zinashuka chini” alisemaa Erick.


Alisema vifaa hivyo ambavyo ni vya maabara ya kupuma damu kwa mama na vya usaidizi wa kupumua kwa watoto wanaozaliwa na changamoto vina umuhimu mkubwa katika kunusuru maisha ya binadamu.


Bakuza alisema kuwa vipo pia vifaa vya kujifunzia vyote vikiwa na lengo la kukabiliana na vifo vya mama na mtoto.


Vile vile aliongeza kuwa USAID Afya Yangu wamekuwa wakishirikiana na serikali katika masuala ya afya na kudai vifaa hivyo vinakwenda kuwa msaada kwenye eneo hilo la mama na mtoto.Akipokea msaada wa vifaa hivyo kwenye kikao cha tathmini ya vifo vitokanavyo na uzazi kwa kipindi cha januari hadi machi Katibu Tawala wa mkoa wa Mara Gerald Kusaya alisema kuwa vifaa hivyo vimetolewa wakati muafaka na vitasaidia ssna kupunguza vifo vya Mama na Mtoto.

Kusaya ameshukuru shirika hilo kama mdau kwa vifaa walivyo vitoa na kuomba kufanyika kwa kipindi kingine huku akitoa wito kwa wadau wengine kushirikiana na serikali katika huduma za afya.


Katibu Tawala huyo wa mkoa wa Mara amewataka wataalamu wa afya kutumia kikao hicho kuja na mpango mzuri wa kukabiliana na vifo vya mama na mtoto.


Kwa Upande wao wananchi wananchi wamesema vifaa hivyo vya maabara pamoja na maboresho ya vituo vya afya uliofanya na serikali pamoja na sekta binafsi utasaidia kuimarisha ulinzi wa mama na mtoto,kabla,wakati na baada ya kujifungua.


“Serikali imeboresha Vituo vya Afya iki ni pamoja na kujenga Hospitali mpya lakini changamoto ni upungufu wa watalaamu pia tunaomba nallo liangaliwe”,  Juma Chacha alisema.


Mpango jumuishi wa tiafa wa malezi,makuzi na maendelo ya awali ya mtoto unaolenga kundi la watoto wa umri wa kati ya miaka 0-8 unasisitiza juu ya uwepo wa miundombinu pamoja na mazingira ambayo yatahakikisha ulinzi na uhai wa mtoto akiwa tumboni,wakati wa kuzaliwa na baada ya kuzaliwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post