NSSF YATUMIA MAONYESHO YA 11 YA BIASHARA NA UTALII KUITANGAZA NSSF TAARIFA

Mkuu wa wilaya ya Muheza Zainabu Abdallah kushoto akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mkuu wa Matekelezo Mkoa wa Tanga Wa MFUKO wa Taifa wa Hifadhi za Jamii nchini (NSSF) Abubakari Mshangama 

MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian kulia akisalimiana na Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga Abubakari Mshangama wakati alipofika viwanja vya shule ya Sekondari Usagara kufungua Maonyesho ya 11 ya Biashara na Utalii

MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batild Burian kulia akipata maelezo kutoka kwa Afisa Matekelezo Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga Abubakari  Mshangama

MKUU wa wilaya ya Muheza Zainab Abdallah akizungumza mara baada ya kutembelea Banda la NSSF mapema leo wakati wa maonyesho hayo






Na Oscar Assenga,Tanga

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi za Jamii nchini (NSSF) wameshiriki maonyesho ya 11 hya Biashara na Utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara Jijini Tanga huku wakiitangaza huduma yao mpya ya NSSF Taarifa.

Akizungumza leo Afisa Matekelezo Mkuu wa NSSF Mkoa wa Tanga Abubakari Mshangama ambapo alisema mpango huo ni muhimu kwa sababu unamuwezesha mwanachama kupata taarifa binafsi ,michango na madai yake.

Alisema huduma hiyo inapatikana kupitia simu ya kiganjani kwa njia tatu ambazo ni ujumbe mfupi (SMS),Programu ya simu ya Kiganjani (Mobile App) ya NSSF na WhatApp.

“Leo tupo hapa kwenye maonyesho haya pamoja na kutoa elimu kuhusu huduma zetu lakini pia tunatumia kuitangaza Programu hii inamuwezesha mwanachama kupata taarifa na huduma mbalimbali kwa njia ya ujumbe mfupi”Alisema

Aidha alisema pia walikuwa wakieleza mafao yanayotolewa na Mfuko huo na vigezo vyake ikiwemo Mafao ya Pensheni ya Uzeeni ambayo mwanachama hulipwa kila mwezi kwa anayetimiza vigezo vilivyowekwa.

Awali akizungumza mara baada ya kutembelea Banda la NSSF Mkuu wa wilaya ya Muheza Zainab Abdallah alisema NSSF ni muhimu sana huku akiendelea kuwashawisha wafanyakazi na wasiowafanyakazi kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na mafao mbalimbali ikiwemo ya matibabu na gharura

Alisema wanapoweka akiba yako inakuwa ni rahisi unapokumbana na changamoto mbalimbali inakuwa ni rahisi kuweza kukuhudumia na kukupa matibabu ikiwemo unapofikia umri wa kustaafu unaweza kujilea mwenyewe.

“Niendelee kuwahimiza wafanyakazi na waajiri wajue kwamba ni takwa la kisheria wahakikisha wanawaingiza watumishi kwenye mfuko wa hifadhi za Jamii (NSSF) ili kuweza kunufaika na huduma mbalimbali”Alisema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post