NAIBU WAZIRI BYABATO ASHIRIKI MKUTANO WA 44 WA BARAZA LA KISEKTA MBALIMBALI LA MAWAZIRI

Mkutano wa 44 Wa Baraza la Kisekta La Mawaziri wa Viwanda, Biashara, Uwekezaji na Fedha (SCITIF) la Jumuiya ya Afrika Mashariki umefanyika 31 Mei, 2024 jijini Arusha Tanzania. Mkutano huo ulitanguliwa na mikutano ya ngazi ya watalaam na Mkutano wa Makatibu Wakuu iliyofanyika kuanzia tarehe 27 hadi 30 Mei 2024.

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo uliongozwa na Mhe. Mwigulu Nchemba (Mb.), Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Viongozi wengine walioshiriki ni Mhe. Sharif Sharif, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Stephen Byabato (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mhe. Exaud Kigahe, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara.

Mkutano huo ulipokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa maamuzi ya mkutano wa 43 wa SCITIF, taarifa ya mashauriano ya Kibajeti wa Mawziri wa Fedha wa Jumuiya, taarifa ya Kamati za Forodha, Biashara, Uwekezaji, Viwango vya Afrika Mashariki na taarifa ya Mamlaka ya Ushindani ya Afrika Mashariki. 

Katika Mkutano huo ujumbe wa Tanzania ulieleza Serikali ya Kenya kufanya haraka kuajiri maafisa watakaokamilisha taratibu za kiforodha zinazotakiwa ili kuclear mizigo ya wafanyabiashara kutoka Tanzania wanaosafirisha mizigo yao kwenda nchini Kenya ili kuondoa usumbufu ambao umekuwepo kwa muda mrefu. Vilevile, Tanzania na Kenya zimekubaliana kutoza viwango sawa vilivyoidhinishwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa magari yanayovuka mipaka ya nchi hizo mbili.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post