MATUMIZI HASI YA TEKNOLOJIA CHANZO CHA MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU KWA WASICHANA

 

Na Dotto Kwilasa, Dodoma

Kiwango cha maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI kwa kundi la vijana wa kike wenye umri wa kuanzia miaka 15 hadi 24 kimeongezeka kutoka asilimia 0.14 kwa mwaka 2016/2017 hadi asilimia 0.33 kwa mwaka 2022/2023 huku sababu mbalimbali zikitajwa ikiwemo matumizi hasi ya teknolojia. 

Hatua hii inatokea licha ya kiwango cha maambukizi mapya kutajwa kuendelea kupungua kwa makundi yote,kutoka watu 72,000 mwaka 2016/2017 hadi kufikia watu 60,000 kwa mwaka 2022/2023 idadi ambayo sawa na punguzo la asilimia 16.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt. Jerome Kamwela ameeleza hayo leo June 7,2024 Jijini Dodoma kwenye mkutano wake na vyombo vya habari kuhusu hali ya maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kwa vijana wa kike. 

Dkt. Kamwela ameeleza kuwa TACAIDS kwa kushirikiana na wadau imeendelea kutekeleza afua mbalimbali zinazowalenga vijana wa umri wa miaka 15-24 waliopo shuleni na wale walio nje ya shule ili kuwapatia elimu ya stadi za maisha kuondokana na ushawishi utaopelekea kupata maambukizi. 

Amesitaja baadhi ya afua hizo kuwa ni pamoja na zile zilizotekelezwa kwa kuwahusisha vijana balehe na wanawake (AGYW)kupitia mradi wa Timiza malengo wa DREAMS ili kuwapatia elimu ya VVU na Ukimwi, afya ya uzazi na stadi za maisha, wasichana walio nje ya shule wakewezeshwa kiuchumi na kuwa salama . 
Kuhusu visababishi vya kupanda kwa maambukizi hayo kwa wasichana,Dkt .Kamwela amesema matumizi mabaya ya teknolojia yanayofanywa na mabinti huchochea na kuongeza ushawishi wa ngono zembe pamoja na kutokuwa na uelewa wa kutosha wa mbinu za kujikinga na maambukizi mapya, ndoa za utotoni,utandawazi, tamaa, umaskini na kujihusisha na wapenzi zaidi ya mmoja. 

Amefafanua kuwa utafiti wa viashiria vya VVU na Ukimwi mwaka 2022/2023 kiwango cha ushamiri wa VVU kitaifa ni asilimia 4.4 ambapo kwa wanawake ni asilimia 5.6 na wanaume asilimia 3.0.

"Hii inamaanisha kwamba jumla ya watanzania 1,548,000 wanaishi na maambukizi  ya VVU , umri wenye kiwango kikubwa cha ushamiri kwa wanaume ni miaka 50-54 kwa wanawake ni miaka 45 hadi, " ameleeza





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post