BYABATO AZIDI KUIPA NGUVU MICHEZO JIMBONI


Wachezaji wa Timu zote mbili kabla ya mchezo
Mbuzi wa zawadi waliotolewa na Mh Mbunge Adv Stephen Byabato
Katibu wa Mbunge Eng Pasaka  Bakari (Aliyevaa kofia ya kijani ) akifuatilia mchezo maalum wa mpira


 Na Mariam Kagenda_ Kagera

Siku Chache Baada ya Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Wakili Stephen Lujwahuka Byabato kutoa zawadi ya Pesa Taslimu kwa washindi wa mchezo wa SNOOKER katika fainali zilizofanyika Ukumbi wa Bukoba Club kwa mara nyingine Mhe. Mbunge Byabato ameunga Mkono Mchezo wa kirafiki wa hisani kwa Kutoa Zawadi ya Mbuzi Wawili kwa Timu za mpira wa miguu za Tydo Academy na Stendi Chama ya Loto.

Timu hizo mbili zimekutana katika Mchezo wao maalum wa Kusherehekea Siku ya Eid uliopigwa katika nyasi bandia za Kaitaba na mechi kumalizika kwa Tydo Kuibuka kidedea, mara baada ya ngwe hiyo kutamatika Katibu wa Mbunge Ndg. Pasaka Bakari amekabidhi mbuzi Wawili kwa manahodha wa Timu zote Mbili ikiwa ni Zawadi Kutoka kwa Mhe. Byabato ambaye alialikwa kama Mgeni Rasmi lakini hakuhudhuria Kutokana na kutokuwepo Jimboni.

Mhe. Byabato ameendelea kuunga mkono Michezo kila inapobidi kufanya hivyo katika Mashindano mbalimbali, huku macho na masikio ya walio wengi wakisubiri Ligi ya Jimbo itakayoanza kutimua vumbi Mwezi Ujao

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post