MTOTO MWENYE UALBINO AIBIWA NA WASIOJULIKANA.. DC NYAMAHANGA ASEMA ZOEZI LA KUMTAFUTA LINAENDELEA

Mkuu wa wilaya ya Muleba Dkt Abel Nyamahanga akimpa pole mama wa mtoto aliyepotelewa na mtoto wake
Mkuu wa wilaya ya Muleba Dkt Abel Nyamahanga akizungumza na wananchi baada ya kufika eneo alikoibiwa mtoto mwenye ualbino

Na Mariam Kagenda _Kagera 


Watu  ambao bado hawajafahamika wamemuiba  mtoto mwenye ualbino mwenye umri wa miaka miwili na nusu katika Kijiji cha Bulamula Kata ya Kamachumu Wilayani Muleba mkoani Kagera kisha kutokomea naye kusikojulikana.


Mama wa mtoto huyo ambaye ni Judith Richard amesema kuwa tukio la kuibiwa kwa mtoto wake wa kike  aitwaye  Noela Asimwe Novath
 limetokea nyumbani kwake Mei 30 mwaka 2024 majira ya saa moja jioni na mtoto huyo ni 

Bi. Richard  amesema kuwa walikuwa wanaume wawili ambapo mmoja alikuja kuomba msaada wa chumvi  na baada ya  kutoka  nje alikabwa na watu hao kisha wakamchukua mtoto wake na kukimbia naye hivyo ameomba Serikali kumsaidia kumtafuta mtoto wake ili aweze kupatikana .

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kamachumu Bwana Leodigad Chonde amesema kuwa tayari wameanzisha ulinzi shirikishi kwa kushirikiana na Jeshi la polisi wa kumtafuta kila sehemu ya Kata hiyo lengo ni kuhakikisha mtoto huyo anapatikana akiwa salama .

Katibu wa chama cha watu wenye ualbino Wilaya ya Muleba Bw. Mahamudu Musedemi ameomba Serikali wilayani Muleba kuhakikisha wanamtafuta mtoto huyo kwani kitendo hicho kinawafanya kuishi kwa hofu.

Mkuu wa Wilaya ya Muleba Dkt. Abel Nyamahanga amesema Serikali ipo inaendelea na zoezi la kuhakikisha mtoto huyo anapatikana akiwa hai na kuwaomba  Wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa jeshi la Polisi ili mtoto huyo aweze kupatikana.

Aidha amesema kuwa kitendo hicho sio kizuri na kinatakiwa kukemewa na kila mtu na kuwaomba kuhakikisha  kila mmoja kwa nafasi yake anashiriki kutafutwa kwa mtoto huyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post