TPDC YAPONGEZWA KUENDESHA VIWANDA VYA KUCHAKATA GESI KWA KUTUMIA WAZAWA

Wajumbe wa  Bodi ya Wakurugenzi TPDC wamepongeza jitihadaa zinazofanywa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika kuwajengea uwezo wafanyakazi wanaoendesha mitambo ya kuchakata gesi asilia Songosongo na Madimba ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi ndani na nje ya nchi, hii imewezesha wafanyakazi hao kuwa na uwezo mkubwa wa kuendesha mitambo hiyo.

Akiongea katika ziara hiyo, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Mjiolojia Bwana Salavatory Ntomola alisema “Ni jambo la kujivunia kwa TPDC na Nchi kuona mitambo hii ikiendeshwa na watanzania kwa asiliamia mia moja’’.

#TunawezeshaMaisha

 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post