WIZARA, TCRA, MAELEZO KUJADILIANA NAMNA YA KUJIBU TAARIFA ZA MITANDAONI

 

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea Ofisi za JamiiForums, Jijini Dar es salaam.
                                                 ************
Na Mwandishi Wetu.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Nape Nnauye  amesema anatarajia kuzungumza na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Idara ya Habari  MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali ili  kuweka miundombinu ya kupokea maoni na mapendekezo ambayo yatafanyiwa  kazi haraka na kuifanya Jamii kuwa na usalama na utulivu dhidi ya taarifa zisizo sahihi.

Akizungumza Jijin Dar es saalaam juzi wakati alipotembelea Ofisi za JamiiForums, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Nape  Nnauye amesema Serikali inaamini katika uhuru wa Watu kujifanyia maamuzi wenyewe.

Amesema mazungumzo hayo yatahusisha kuweka “mechanism” ya kushirikiana ili kuhakikisha taarifa sahihi zinafanyiwa kazi ndani ya muda mfupi na Wananchi kujulishwa

Amesema “Ni rahisi mtu kuja na taarifa ya uongo na kupoteza mwelekeo kwa Wananchi zaidi ya milioni 60. 

Sisi (Wizara) tutakuwa mabalozi wa JamiiForums ili mfanye kazi na Wadau mbalimbali kwa kuwa wote tuna lengo moja,amesema Nape

Amesema wakati mwingine Wanasiasa au viongozi hudhani wanajua zaidi kuliko Wananchi lakini ukweli ni kuwa Wananchi wanajua wanachokitaka, wanatakiwa tu kupewa taarifa sahihi.

Katika hatua nyingine amesema “Nimefurahi kuja JamiiForums sikuwa najua kama mna ukubwa wa kiasi hiki, kwa mambo mnayoyafanya ninyi ni Wadau wangu wa muhimu sana, mnafanya kazi kubwa, mna historia yetu ambayo ni nzuri na vizuri mkaendelea kuitunza.”

Ameongeza “Moja kati ya malengo ya Wizara ni kuhakikisha Jamii inakuwa na taarifa sahihi kwa sababu tunaamini ikiwa na taarifa sahihi za kutosha itakuwa chachu ya wao kujiletea maendeleo na kutatua matatizo yao ya msingi ikiwemo Afya, Elimu na mengine mengi.”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo, amesema wana mpango wa kutengeneza simu janja Zaidi ya millioni 10 kwa miezi tisa ijayo ambayo itaenda kuwasaidia wananchi walio vijijini  hususani vijana na wanawake zinazotarajiwa kuuzwa kwa bei ya chini ya elfu 50.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa  habari alipotembelea Ofisi za JamiiForums, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye, na Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo, wakifurahia jambo mara baada ya kupiga picha ya pamoja wakati waziri nape alipotembelea ofisi za Jamiiforums.

Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo, na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye, wakisalimiana mara baada ya kuwasili kwa waziri huyo katika Ofisi za Jamiiforums jijini Dar es salaam.





 Picha mbalimbali wakati Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye, alipotembelea Ofisi za JamiiForums, jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa Jamiiforums, na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye, katika ofisi za jamiiforums. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post