WANAFUNZI VYUO VIKUU WAPONGEZA BAJETI YA ELIMU KUONGEZA WANUFAIKA WA MIKOPO

Wanafunzi wa elimu ya juu wameipongeza Serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mabadiliko makubwa waliyofanya kwenye sekta ya elimu huku wakitoa wito kwa wanafunzi wanaopata ufadhili Samia Skolashipu kusoma kwa bidii ili waweze kusaidia jamii katika siku zijazo.


Rai hiyo imetolewa na mwanafunzi kutoka Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi (Muhimbili), Yuda Sale ambaye pia amepongeza uongezwaji wa wafanyakazi katika vyuo akisema unachangia kuongeza ufaulu wa wanafunzi kwa kiwango kikubwa.

Kwa upande wake Alice Robert, mwanafunzi kutoka Taasisi ya Uasibu Tanzania (TIA) amepongeza utekelezaji wa bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24 akisema wana matarajio makubwa kuwa kupitia bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 mageuzi makubwa katika sekta ya elimu yataenda kufanyika na kwamba wanafunzi watasoma katika mazingira bora zaidi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post