TGNP YATOA MAFUNZO YA URAGHIBISHI KWA WANANCHI WILAYANI MWANGA, WENYEWE WAELEZA KUSHAMIRI KWA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA

Mwezeshaji wa mafunzo kutoka Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP), Schola Makwaia akitoa mafunzo ya uraghibishi kwa wananchi wa Kata ya Lembeni Wilayani mwanga Mkoani Kilimanjaro.

****

Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) umetoa mafunzo ya uraghibishi kwa wananchi wa Kata ya Lembeni Wilayani Mwanga, ambayo yamelenga kuwajengea uwezo wa kushiriki, kuchambua kwa kina changamoto zinazowakabili katika mazingira yao na kuzitafutia ufumbuzi.
 
Mafunzo hayo yanatumia uraghibishi kama mbinu ya utafiti shirikishi ili kupata changamoto zinazokabili wananchi, ambapo kupitia mafunzo hayo wameweza kubaini kushamiri kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye Kata hiyo ikiwemo ubakaji na ulaiwiti kwa Watoto.
 
Mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka TGNP Schola Makwaia anasema baada ya wananchi kuibua  changamoto hizo wameweza, kuzichambua na kuzitafutia utatuzi, kwa kutengeneza mpango kazi kwa ajili ya ufuatiliaji.
 
“Tumekuja kusikiza zaidi kutoka kwa wananchi ambapo tumepata mambo mbalimbali hivyo tumetengeneza mpango kazi ambao wananchi watashirikiana na viongozi, na baaadae tutaanzisha kituo cha taarifa na maarifa na kitaanza kufanyia kazi changamoto hizo kwa kutumia mpango kazi huo”,  anasema Schola.
 
Wananchi walioshiri mafunzo hayo wamesema elimu waliyopatiwa itasaidia kumaliza changamo zilizopo kwenye Kata ya Lembeni ya kukithiri kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji na ulawiti.
 
Wanasema kwa upande wa hali ya wanawake na uongozi, wamepiga hatua kwa kuwa na viongozi wanawake, hivyo eneo linalohitaji kupewa kipaumbele ni suala la ukatili wa kijinsia ili kutokomeza vitendo hivyo.

Mwezeshaji wa mafunzo kutoka Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP), Schola Makwaia akitoa mafunzo ya uraghibishi kwa wananchi wa Kata ya Lembeni Wilayani mwanga Mkoani Kilimanjaro.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post