![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiVfDVeGG-j-XXANHYF4thdHP7NhTg9yIy4wrSut82RgWZOViWRDEWw2GZrcHOeSS41wG6-KPiCibJo93KviVrFQ0hrMocwlEQG6lSsLkz2GFX56F6t5Xs9DItZeJCd6PAVVfcCCsriQnbn15qNqWAc-0Kjgigko91iAryLViNk84A9mopgBA5nUdGcNg/w640-h426/IMG-20240502-WA0092.jpg)
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka 2024/2025 amesema kuwa uzalishaji wa chakula kwa msimu wa kilimo wa 2022/2023 ulitosheleza mahitaji ya chakula ya tani 16,390,404 kwa mwaka 2023/2024 na kuwepo kwa ziada ya tani 4,011,611.
Amesema kutokana na hali hiyo, Taifa limejitosheleza kwa chakula kwa asilimia 124 ikilinganishwa na utoshelevu wa asilimia 114 mwaka 2022/2023. Aidha, utoshelevu wa chakula unatarajiwa kufikia asilimia 130 ifikapo mwaka 2025.