MUHALILA ADHAMINI VIFAA VYA MICHEZO MASHINDANO YA UMITASHUMITA NA UMISSETA MULEBA

Mkuu wa wilaya ya Muleba Dkt Abel Nyamahanga akikabidhi vifaa vya michezo vilivyotolewa na Muhalila
Na Mariam Kagenda_Kagera 

Mdau wa michezo ambaye ni Mkurugenzi wa Mashindano ya Muhalila Cup Fortunas Muhalila  amedhamini Mavazi ya Wanafunzi ambayo ni    Traksuti 100  pamoja na Traksuti 13 za viongozi na walimu wa michezo katika mashindano ya UMITASHUMITA kwa shule za Msingi na UMISSETA  kwa mwaka 2024 ili kuwawezesha  Wanafunzi wa Wilaya ya Muleba kushiriki mashindano hayo kwa kujiamini.

Vifaa hivyo vya michezo vilikabidhiwa kwa niaba yake na Diwani wa kata ya  Izigo Edwin Kaena kwa mkuu wa Wilaya ya Muleba  Dkt  Abel Nyamahanga  ambaye alisema mdau huyo wa michezo amekuwa nguzo muhimu katika kuhakikisha Wilaya hiyo inaendelea kupiga hatua kimichezo na kusema kuwa ataendelea kushiriki katika harakati mbalimbali za maendeleo  ili kurudisha  shukrani kwa jamii yake ambayo ilimfunza na kumlea.

Msemaji wa Muhalila Cup Omary Rwakaya amesema  kuwa licha ya udhamini huo wa  mashindano ya  UMISETA na UMITASHUMITA pia  waliwai  kutoa  mipira na vifaa vya michezo katika shule 70 za Wilaya ya Muleba  ili kuendelea kukuza michezo na kuibua vipaji vya watoto.


Mkuu wa Wilaya ya Muleba Dr Abel Nyamahanga alitoa shukrani kwa mdau huyo wa maendeleo kwa kuwa mdhamini na kuthamini michezo huku akiwahakikishia wadau na walimu wa michezo kuwa Halmashauri hiyo  itaendelea kutenga fedha  kwa ajili ya kuendeleza michezo na mashindano hayo kwa ujumla huku akitoa onyo kwa  walimu wanaowazuia Wanafunzi kushiriki   michezo kwa kisingizio kuwa wanavipindi vingine .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post