BENKI YA NBC YAKUTANA NA WAFANYABIASHARA, WADAU SEKTA YA BENKI KUJADILI FURSA ZINAZOPATIKANA NBC

Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Shinyanga, Bi. Joyce Chagonja
akitoa elimu katika warsha ya wafanyabiashara na wadau wa sekta ya benki .

Na Mwandishi wetu Malunde 1 Blog

Benki ya Taifa ya Biashara ya NBC tawi la Shinyanga imekutana na wafanyabiashara na wadau wa sekta ya Benki na kuwapa elimu ya Fedha pamoja na fursa zinazopatikana katika benki hiyo.

Elimu hiyo imetolewa katika warsha iliyofanyika leo Alhamis Mei 23,2024 katika Ukumbi wa Vigmark Hotel Mjini Shinyanga ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya fedha, kuimarisha ushirikiano , kufahamiana pamoja na kuwaeleza fursa zinazopatikana katika Benki hiyo.

Akizungumza wakati wa warsha hiyo , Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Shinyanga, Bi. Joyce Chagonja amesema Benki ya NBC ambayo ni Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC Premier League) na NBC Championship ina fursa zinazopatikana katika Benki hiyo ikiwemo Bima za afya na vyombo vya moto, mikopo pamoja na akaunti mbalimbali ikiwemo Akaunti ya Mshahara, Akaunti ya Kua Nasi, Akaunti ya Malengo ,Account ya jamii ambayo haina makato (Free Banking ) na Akaunti ya NBC Direct na huduma za NBC Wakala.

Aidha Chagonja amewashauri wafanyabiashara na wadau wa sekta ya Benki kuendelea kujiwekea akiba ,kufanya uwekezaji pamoja na kuwa na bima katika Benki ya NBC wakati wa kufanya biashara zao.

“Tumekutana hapa leo ili kuwaeleza huduma tulizonazo katika benki yetu ya NBC ili muweze kuzifahamu fursa zinazo patikana katika benki yetu ya NBC ikiwa ni pamoja na kuimarisha mahusiano baina yetu na ni nyie wafanyabiashara na wadau wa sekta ya benki katika Tawi letu la Shinyanga pia niwaahidi kuwa ,tutaendelea kushirikiana ili kuhakikisha tunatatua changamoto zinazoikabili katika biashara zenu.

Tunazo huduma nyingi za kifedha. Karibuni Benki ya NBC pia mfurahie njia mbadala za kupata huduma za kibenki ‘Benki Kidijitali na NBC’ bila ulazima wa kufika kwenye tawi kwa kupiga *150*55# au kupitia App ya NBC Kiganjani pamoja na   NBC CONNECT ”,amesema Chagonja.

Pia katika warsha hiyo Meneja biashara na mahusiano kwa Wateja wakati na wakubwa wa benki ya NBC, Carlos Kapinga ametoa elimu ya vigezo vya kupata Mikopo ya Magari,Mashine ,Majengo ya biashara na vifaa vya biashara kwa wafanyabiashara na wadau wa sekta ya Benki walioshiriki katika warsha hiyo ambayo ni Mikopo yenye riba nafuu kwa wateja.

Kwa upande wake, Mdau wa sekta ya Benki Jakton Koy ambaye ni mkurugenzi wa Shule za Kom Schools ameupongeza uongozi wabenki ya NBC kwa kuamua kukutana na wafanyabiashara na wadau wa sekta ya benki na kuwapa elimu na kuwaeleza fursa zinazopatikana ktika benki hiyo huku akiwashauri kuendelea na utaratibu huo wakuwafikia wananchi na kuwapa elimu ya fedha namna ya kutunza fedha zao hali itakayo waepusha na kujiingiza katika mikopo umiza.

Baadhi ya washiriki wa Warsha hiyo wameishukuru Benki ya NBC kwa kuwajali na kuwapata mafunzo hayo ambayo yatawasaidia kuwa na nidhamu ya fedha lakini pia kuweka akiba na kufanya uwekezaji kupitia benki hiyo.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Shinyanga, Bi. Joyce Chagonja akizungumza na wafanyabiashara na wadau wa sekta ya benki mkoa wa Shinyanga.
Maafsa wa Benki ya NBC Tawi la Shinyanga wakishiriki katika warsha ya wafanyabiashara na wadau wa sekta ya benki mkoa wa Shinyanga.
Wafanyabiashara na wadau wa sekta ya benki mkoa wa Shinyanga wakiwa katika warsha iliyoandaliwa na Benki ya NBC Tawi la Shinyanga.

Wafanyabiashara na wadau wa sekta ya benki mkoa wa Shinyanga wakiwa katika warsha iliyo andaliwa na Benki ya NBC Tawi la Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post