MBUNGE LUCY MAYENGA ATOA MABATI 100 KUKAMILISHA UJENZI WA ZAHANATI IBOJA - KISHAPU


Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe.  Lucy Mayenga amewashika mkono wananchi wa kata ya Mwakipoya wilayani Kishapu kwa kuwachangia mabati 100 yenye thamani ya Shilingi Milioni 3,600,000/= kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Iboja.

Mhe. Mayenga ametoa mchango huo leo Mei 18, 2024 katika Kijiji cha Iboja kata ya Mwakipoya wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Pia Mhe.  Lucy Mayenga amekabidhi matairi 6 ya gari yenye thamani ya Shilingi Milioni 2,400,000/=  kwa Jeshi la polisi wilaya ya Kishapu katika kuunga mkono jitihada za jeshi hilo kuimarisha ulinzi wa raia na mali zao.


Akizungumza wakati wa kukabidhi mabati na matairi hayo, Mbunge viti maalum Mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Lucy Mayenga ametoa mabati 100 yenye thamani ya Milioni 3,600,000/= kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Iboja na kuwaahidi kikundi cha akina mama wa kijiji hicho kuwapatia mtaji wa vyombo ili waweze kujiinua kiuchumi.

"Kilio kikubwa cha wananchi wa kijiji cha Iboja na kata ya Mwakipoya ni upatikanaji wa huduma za afya hususani kwa akina mama pindi wanapohitaji kujifungua, kupitia risala hii na maombi yaliyowasilishwa na Mheshimiwa diwani wenu natoa mabati 100 yenye thamani ya Shilingi Milioni 3,600,000/= ili yaweze kutumika kumalizia ujenzi wa zahanati ya Iboja, suala la huduma za afya ni kipaumbele kikubwa katika utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi ndio maana Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuboresha miundombibu, madawa pamoja na  wataalam kwenye sekta ya afya", amesema Mhe. Mayenga.


"Nitaendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na wananchi katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu lengo ni kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga", ameongeza Mhe. Mayenga.

Akitoa shukrani kwa niaba ya wananchi mara baada ya kukabidhiwa mabati hayo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi tawi la Iboja Michael Izengo amemshukuru Mbunge Lucy Mayenga kwa kuwashika mkono wananchi wa kata ya Mwakipoya.


"Kukamilika kwa zahanati hii ilikuwa ni jambo la kihistoria kwa wakazi wa kijiji cha Iboja na leo Mheshimiwa Mbunge wetu Lucy Mayenga ameandika historia kubwa kwa vizazi na vizazi, tunamshuru sana na tunaahidi kuendelea kushirikiana na viongozi wetu akiwemo Rais wetu Samia Suluhu Hassan", amesema Izengo.

Akisoma taarifa wakati wa mkutano wa hadhara juu ya hali ya upatikanaji wa huduma za afya kwenye kijiji cha Iboja mtendaji wa kijiji cha hicho Alphonce Gunda amesema kumekuwa na changamoto ya muda mrefu ya ukosefu wa zahanati hali inayopelekea kufuata huduma za matibabu umbali mrefu.


"Dhumuni la kuanzisha ujenzi wa zahanati ni kuongeza upatikanaji wa huduma kwenye kata yetu kwa sababu kata yetu ina vijiji vinne lakini zahanati na moja, hivyo kukamilika kwa ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Iboja kutaondoa changamoto ya kujifungulia njiani kwa akina mama kutokana na umbali wa kilometa 13 wakifuata huduma", amesema Gunda.

"Changamoto ya upatikanaji wa huduma za afya ilitulazimu kuanzisha ujenzi wa zahanati kwenye kwa nguvu za wananchi, ambapo mnamo mwaka 2018 tulianza ujenzi kwa michango ya fedha za wananchi na nguvu kazi, mpaka sasa wananchi wameendelea kujitolea kusomba mchanga, maji na mawe, hivyo tunakuomba Mheshimiwa Mbunge Lucy Mayenga utushike mkono ili tuweze kukamilisha ujenzi huu na wananchi hususani akina mama waweze kupata huduma za afya karibu", ameongeza Gunda.

Baadhi ya wananchi wa kata ya Mwakipoya waliojitokeza kwenye mkutano huo.

Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga akikabidhi mabati kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Iboja.

Diwani wa kata ya Mwakipoya Tabitha Sodikiel akizungumza wakati wa mkutano huo.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga akizungumza na wananchi wa kata ya Mwakipoya.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi  (UWT) Mkoa wa Shinyanga Grace Samweli akizungumza wakati wa mkutano huo,
Diwani Viti Maalum wilaya ya Kishapu Devotha Jilala akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kjiji cha Iboja Joseph Kulwa akizungumza wakati wa mkutano huo.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga akipokelewa na wakazi wa kata ya Mwakipoya.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga akipokelewa na wakazi wa kata ya Mwakipoya.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga akikabidhi taili za magari kwa Kaimu mkuu wa kituo wilaya ya Kishapu SGT. Grace Samson.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post