LHRC YAWAPIGA MSASA WANAHABARI

*****
Na Mwandishi Wetu -Dodoma

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimewapa semina ya siku mbili kwa waandishi mbalimbali wa habari hapa nchini yenye lengo la kuwajengea uelewa juu ya taarifa zinazohusu mauaji ya wenza.

Semina hiyo imeanza leo jijini Dodoma, huku pia ikilenga kuwapa elimu hiyo ambayo itakuwa chanya katika kuandika habari zinazohusu mauaji ya wenza ,ukatili wa kijinsia,Viashiria hatarishi vya ukatili.

Kwa siku ya kwanza Mafunzo hayo yatahusu madhara ya mauaji ya wenza , maana ya mauaji ya wenza kwa Tanzania,Taarifa ya ripoti maalumu ya mauaji ya wenza ,Taarifa ya Haki za Binadaamu kuhusu mauaji ya wenza jinsi athari zake zinavyoathiri makundi mbalimbali.


Katika hatua nyingine kwa siku ya pili mafunzo hayo yatahusu Sheria kuhusu ukatili na mauaji ya wenza,utoaji habari zenye kuzingatia hali ya wahanga na mifano ya habari mbalimbali nzuri na mbaya lugha nzuri ya kutumia masuala ya jinsia.













(PICHA ZOTE NA JOHN SIMWANZA)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post