RC MACHA AWEKA MKAZO KILIMO CHENYE TIJA ZAO LA PAMBA

 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akiwasaidia Wakulima wa Pamba kupima Pamba yao katika AMCOS ya Kishapu.


Na Marco Maduhu,KISHAPU

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha,amewataka Wakulima wa Zao la Pamba mkoani humo kuacha kulima kimazoea,bali walime kilimo chenye tija kwa kufuata ushauri kutoka kwa Wataalamu, ili walime kisasa na kupata mavuno mengi na kuinuka kiuchumi.

Amebainisha hayo leo Mei 23,2024 wakati alipofanya ziara wilayani Kishapu, kutembelea baadhi ya Vituo vya Mauzo ya Pamba kupitia Vyama vya Msingi vya Ushirika AMCOS.
Amesema siyo kweli zao la Pamba linamtupa Mkulima,lakini wakulima wanavyolima ndiyo tatizo, kutokana na Kulima kimazoea na kupata Mavuno machache.

"Rais Samia alivyoniapisha,alinipa Maelekezo kuja kusimamia Zao la Pamba, ili kiwe Kilimo chenye Tija na kuwainua Wakulima Kiuchumi,"amesema Macha na kuongeza,

"Hapa Kishapu ninataarifa kwamba wananchi hua mnalima Kimazoea na kupata Kilo 200 kwa Hekali Moja, ambapo Mkulima Kitaalamu,Hekali Moja Mnaweza kupata Kilo zaidi ya 1,800 hadi 2,000".
Amewataka Wakulima kuwatumia Maafisa Ugani kupata elimu ya Kilimo chenye Tija,huku akitoa Maelekezo kwa Maafisa gani nao wawatembelee Wakulima mara kwa mara Mashambani mwao na kutoa elimu ya kilimo cha kisasa,sababu Serikali imeshawapatia vifaa vya usafiri.

Amewataka pia Wakulima pindi wanapokwenda kuuza Pamba yao, wahakikishe inakuwa safi na kutoichafua kwa kuweka Michanga au Maji, huku akiwahidi kwamba Serikali itaendelea kuboresha bei nzuri ya Pamba ambayo kwa sasa Kilomoja ni Sh.1150.
Aidha, amewasihi Wakulima kwamba wanapokuwa wakiuza Pamba yao, wazitumie fedha kwa Matumizi Mazuri ikiwamo kununua Chakula,kusomesha Watoto pamoja na kuboresha Makazi yao kwa kujenga nyumba nzuri na za kisasa.

Naye Mmoja wa Wakulima wa Pamba Charles Mashenene,amekiri ni kweli Wakulima wamekuwa wakilima kimazoea kutokana na kutopata elimu ya Kilimo cha kisasa, huku wakilalamikia pia Madawa kutoua Wadudu ambao hushambulia Pamba,na hivyo kusababisha Mavuno kuwa machache licha ya kulima kizamani.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza na Wakulima wa Pamba.
Meza Kuu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akikagua Mezani ya kuuzia Pamba.
Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha.
Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha.
Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha.
Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha.
Wananchi wakiendelea kumsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha.
Wananchi wakiendelea kumsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post