TGNP YAWAKUTANISHA WANANCHI WA LEMBENI NA UONGOZI WA WILAYA MWANGA


Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), umewakutanisha wananchi wanaotoka katika Kata ya Lembeni Wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro, na viongozi wa halmashauri hiyo na kuwasilisha changamoto zinazowakabili katika ngazi ya Kata ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.


 Kikao hicho kilichoongozwa na Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii halmashauri ya Mwanga Meriana Sumari, wananchi waliwasilisha  Changamoto walizoziibua katika Nyanja mbalimbali ikiwemo  ushiriki wa wanawake kwenye uongozi, kilimo hai, ukatili wa kijinsia, mabadiliko ya tabia nchi pamoja na huduma za kijamii ambapo baadhi ziliweza kupatiwa majibu na watendaji husika na nyingine kuahidi kufanyiwa kazi.

Akiwasikisha changamoto hizo mbele ya Kikao hicho Janneth Mshana mkazi wa Kijiji cha Lembeni Kata ya Lembeni amesema waliweza kuibua changamoto walizoziahinisha kwenye makundi makubwa manne baada ya kupatiwa mafunzo ya TGNP, ambapo waliweza kukutanishwa pia na viongozi wa Kata hiyo kabla ya kuzifikiasha ngazi ya Wilaya.


Katika taarifa hiyo wananchi walieleza kushamiri kwa Kwa  matukio ya ukatili ni wa kijinsia ikiwemo unakaji na ukawiti matukio ambayo yanachangiwa na mmomonyoko wa maadili, malezi mabovu kwa wazazi pamoja na kukithiri kwa unywaji wa pombe ukiopitikiza.


Kwa Upande wa uongozi Walisema wanawake wengi wanashindwa kugombea kwa sababu ya kutokujiamini, kukosa elimu  elimu pamoja na majukumu ya kifamilia.


“Wananchi wa Kata Lembeni kwenye Kilimo hususani kilimo hai tumeacha kukitumia tunatumia  kilimo cha kisasa ambacho kinatuletea mabadiliko ya tabia nchi ambayo kutokana na kutumia madawa mengi katika kilimo kwenye mazao ambayo pia yanachangia madawa ardhi kupoteza  rutuba”, amesema Janeth

Mwezeshaji kutoka TGNP Schola Makwaia amesema Wananchi wameweza kuwasilisha changamoto walizoziibua kwa watendaji wa idara husika ambao wamejibu na nyingine kuahidi kuzifanyia kazi.

Amesema baada ya kikao hicho wataanzisha kituo cha taarifa na maarifa kwa ajili ya kuendelea kuzifanyia  kazi  changamoto hizo kwa  kuwekea mpango kazi pamoja na ufuatiliaji katika  utekelezaji wake.

“Tumekuwa kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga kwa zaidi ya siku kumi katika Kata ya Lembeni kwa ajili ya kufanya utafiti shirikishi kutokana na mradi wa wanawake wa vijijini kujiletea mabadiliko,tumekutana na wananchi na makundi tofauti kwa ajili ya kufanya malengo ya mradi ambao umejikita kuangalia hali ya ushiriki wa wanawake katika uongozi, kupambana na ukatili wa kijinsia na kingono, mabadiliko ya tabia nchi pamoja na na kilimo hai.”,amesema Schola.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post