MBUNGE MAVUNDE AJA NA MKAKATI KABAMBE KUWAWEZESHA WANADODOMA


Mbunge wa Dodoma Mjini Mh.Anthony Mavunde, amebainisha kuwa Jimbo lake la Dodoma Mjini litakua linatenga Sh Milioni 20 kila mwaka kwaajili ya kuwawezesha Wananchi kiuchumi kwa ajili ya manunuzi ya mashine na mitambo midogo kwa lengo  la kuzalisha bidhaa na kuongeza thamani kwa bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.

Hayo yamebainishwa leo tarehe  22 Mei 2024 na Mhe Anthony Mavunde (Mb) wakati  akizindua mafunzo ya ujasiriamali yaliyoratibiwa na Jeshi la Polisi pamoja  na Kanisa Halisi la Mungu Baba, Jijini Dodoma. 

“Kutokana na nia ya dhati ya Rais wetu mpendwa Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan  ya kuwainua Wananchi kiuchumi amerejesha tena ile mikopo ya asilimia 10 isiyo na riba na hii itawasaidia kuondokana na mikopo kausha damu.

Ili mkopo huo ulete tija,ni lazima tuwaandae wana Dodoma kupata mafunzo ya ujasiriamali na ujuzi mbalimbali wa uzalishaji bidhaa kupitia mafunzo kama haya ya leo. 

Kwangu kama Mbunge nimekuja na progamu ya kukiinua kikundi kimoja kila mwaka kwa kutoa Tsh 20,000,000 ya ununuzi wa mashine na mitambo kuanzisha viwanda vidogo vidogo”Alisema Mavunde

Kiongozi Mkuu wa Kanisa halisi la Mungu *Baba Askofu Baba Halisi* Ameishukuru Serikali na viongozi wote wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana nao kwa karibu na kueleza dhumuni la mafunzo haya ni kuiandaa jamii kushiriki kikamilifu katika uchumi wa Taifa.

Hapo awali akimwakilisha  RPC Mkoa wa Dodoma Afisa Polisi Jamii Mkoa wa Dodoma Afande Eva Michael Stesheni, ameipongeza Kanisa la Mungu Halisi kwa kuja na wazo hilo la kuwainua Wananchi kiuchumi kwani linaenda sambamba na mipango iliyopo katika Jiji la Dodoma na kwamba kupitia mafunzo haya idadi kubwa ya wanajamii itapata ujuzi wa kushiriki katika uzalishaji mali na hivyo kupunguza vitendo vya uhalifu katika jamii.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post