WANANCHI KAGERA KUNUFAIKA NA FURSA ZA KIUCHUMI UJENZI CHUO KIKUU


Mkuu wa mkoa wa Kagera Fatuma Mwassa akimtunza fedha mpiga ngoma ya asili ya kihaya  wakati wa kumkabidhi eneo mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la chuo kikuu cha Dar_es_Salaam mkoa wa Kagera
Mkuu wa mkoa wa Kagera Fatuma Mwassa akizungumza wakati wa kumkabidhi mkandarasi eneo la Ujenzi wa Tawi la  chuo kikuu cha Dar_es_Salaam mkoa wa Kagera .
Mkuu wa mkoa wa Kagera Fatuma Mwassa(Aliyevaa mtandio mwekundu) akiwa na Naibu makamu mkuu wa chuo cha Dar_es_Salaam na viongozi wengine wa chama na serikali wakati wa kwenda kumkabidhi mkandarasi eneo la ujenzi
Profesa Boniventure Rutinwa Naibu Makamu mkuu wa chuo cha Dar_es_Salaam akizungumza wakati wa kumkabidhi mkandarasi eneo la ujenzi wa Tawi la chuo kikuu cha Dar_es_Salaam mkoa wa Kagera
Mkandarasi kutoka nchini china atakayejenga Tawi la chuo kikuu cha Dar es Salaam mkoa wa Kagera akizungumza wakati wa kukabidhiwa eneo

Na Mariam Kagenda _Kagera

Wananchi mkoani Kagera wanatarajia kunufaika na fursa mbalimbali za kiuchumi baada ya serikali kutoa fedha  kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo kikuu cha Dar_es_Salaam ambao unatarajia kuanza baada ya mkandarasi kukabidhiwa eneo la ujenzi wa chuo leo 

Mkuu wa mkoa wa Kagera Fatuma Mwassa amesema hayo wakati wa kumkabidhi mkandarasi  JIAN XI CORPORATION eneo la ujenzi wa chuo hicho lililopo katika  kijiji cha Itawa  na Kangabusharo kata ya Karabagaine  halmashauri ya wilaya ya Bukoba.

Bi Mwassa amesema kuwa tayari serikali imeshatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo Kikuu cha Da_ss_Salaam katika mkoa wa Kagera  na kuwashukuru wananchi wa kijiji cha Itawa na Kangabusharo kwa kukubali kutoa hekari zaidi ya 300 ili kujenga   chuo hicho  kwa ajili ya maendeleo ya elimu huku akisema kuwa zipo fursa mbalimbali ambazo watanufaika nazo baada ya ujenzi ikiwa ni pamoja na kukuza uchumi wa mkoa huo.


Amesema kuwa fursa nyingine ni pamoja na  Kupanua na kupendezesha mji,Kuongeza marafiki kutoka kwa wageni wanaokuja katika chuo hicho na kuwa na senta ya kutolea mafunzo ya ujasiliamali  ambapo amemtaka mkandarasi huyo kuhakikisha anakamilisha mradi wa ujenzi kwa muda uliopangwa .

Kwa upande wake  Naibu Makamu Mkuu wa chuo Kikuu cha Dar_es_Salaam anayeshughulikia maswala ya Taaluma Profesa Bonaventure Rutinwa  amesema kuwa mradi huo ni sehemu ya mradi mkubwa unaofadhiriwa na serikali kupitia  mkopo wa  World Bank  unaotarajia kughalimu kiasi cha zaidi ya shilingi  bilioni 20 na utajengwa kwa miezi 18.

Ameongeza kuwa majengo yatakayojengwa ni pamoja na Madarasa ,Jengo la utawala , Mabweni ya wasichana na wavulana  pamoja na huduma saidizi zitakazohitajika na kusisitiza wazawa wa maeneo hayo kuchangamkia fursa zitakazojitokeza wakati wa ujenzi na kuwa ujenzi wa chuo hicho utasaidia sana wanafunzi wa mkoa wa Kagera kupata elimu kwa ukaribu pamoja na wanafunzi wengine kutoka mikoa mbalimbali.

Aidha baadhi ya wananchi wa mkoa wa Kagera Josephat Samsoni na wameishukuru serikali kwa namna inavyowakumbuka na kuwajari hasa kwa kuona umuhimu wa mkoa huo kuwa na Tawi la chuo kikuu cha Dar_es_Salaam kwani wanalazimika kuwapeleka watoto wao mikoa mingine ili kupata elimu hivyo baada ya ujenzi huo kukamilika wataondokana na changamoto  hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post