MTOTO WA MIAKA MIWILI ADAIWA KULAWITIWA KAHAMA


Mwenyekiti wa mtaa wa Nyasubi Kahama Leonard Mayala

NA NEEMA NKUMBI HUHESO DIGITAL& HUHESO FM

Mtoto anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 2 hadi miaka 2.5 anadaiwa kulawitiwa na kijana mwenye umri kati ya miaka 15-16 mkazi wa kata ya Nyasubi manispaa ya Kahama Mkoa wa Shinyanga wakati akiwa anacheza nje ya nyumba yao.

Makamu mwenyekiti wa SMAUJATA wilaya ya Kahama Juma Mpei aliyefika katika eneo la tukio ameeleza hatua za awali zilizochukuliwa.

"Tumepokea taarifa kwa kuna mtoto amelawitiwa na mama amebaini baada ya kukuta njia ya haja kubwa kuna uchafu na damu na hatua za awali tulizochukua tumewakamata watuhumiwa na tunawapeleka polisi", amesema.

Mwenyekiti wa mtaa huo Leonard Mayala amekiri kutokea kwa tukio hilo kwenye mtaa wake na kuwataka wazazi au walezi kuwa makini na watoto wao.

Kaimu kamanda wa polisi mkoani Shinyanga Kenedy Mgani akizungumza kwa njia ya simu ameeleza kuwa bado halijafika mezani kwake, analifuatilia na kuahidi kulitolea taarifa kamili baadae.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post