RC MACHA ATAKA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI SHINYANGA, AONYA KUNYIMWA TAARIFA 'MSIKUMBATIE WAGOMBEA"

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Mkoani humo.

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha,amewahidi Waandishi wa habari mkoani humo kwamba kutakuwepo na Uhuru wa Habari wa kutosha kwa maslahi mapana ya wananchi kupata taarifa mbalimbali.

Macha amebainisha hayo leo Mei 15,2024 kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari,ambapo Klabu ya Waandishi wa Mkoa wa Shinyanga (SPC) imeadhimisha leo na Kitaifa Maadhimisho hayo yalifanyika Mei 3 mwaka huu Jijini Dodoma na Mgeni Rasmi alikuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Uhuru wa habari.

Amesema katika Mkoa wa Shinyanga kutakuwepo na uhuru wa habari wa kutosha, na kwamba Taasisi yoyote ile ya Umma ama kiongozi atakaye Mnyima Mwandishi wa habari taarifa, awasiliane naye ili kuliona namna ya kulitatua sababu Habari ni kwa Maslahi ya wananchi.

“Mimi sijawahi kunyima Mwaandishi wa habari Taarifa katika uongozi wangu tangu nilipokuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama na sasa ni Mkuu wa Mkoa Shinyanga, kama yupo ambaye anasema niliwahi kumyima habari anyooshe Mkono,”amesema Macha.
Aidha, amesema kama kuna tatizo la kunyimwa taarifa waandishi mkoani humo analikemea, na kutoa Maagizo kwa Viongozi wa Serikali kwamba wao ni Watumishi wa wananchi na wanawategemea kupata taarifa za Serikali kupitia Waandishi wa habari, hivyo ni vyema wasifiche taarifa bali wazitoe kwa maslahi ya umma.

Amesema kwa zile habari ambazo niza siri kwa maslahi mapana ya nchi ni vyema zisiandikwe,lakini zile ambazo zinagusa maslahi ya wananchi haina haja kuficha taarifa hizo bali waandishi wa habari wapatiwe na kuhabarisha umma.
Amewataka pia waandishi wa habari kwamba katika uhuru huo wa kujieleza wawe na mipaka, pamoja na kufanyia utafiti taarifa zao na kubalance ili kuondoa Migogoro na kusababisha chomba chake cha habari kuomba radhi kwa mdau na kukipunguzia uaminifu.

Uchaguzi Serikali za Mitaa.

Macha amewataka waandishi wa habari mkoani humo, kwamba katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu,wasikumbatie wagombea na kuandika habari za mtu binafsi, bali wajikite kuandika habari kwa maslahi ya umma na wasitumike pia kumchafua Mgombea mwingine.
Ujumbe kwa Wamiliki vyombo vya habari.

Ametoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya habari, kwamba wajali maslahi ya watumishi wao kwa kuwapatia Mikataba na Mishahara mizuri ili wafanye kazi zao kwa ufanisi na kuzingatia maadili ya taaluma yao.

Utunzaji wa Mazingira.

Amewasihi Waandishi wa habari kutumia kalamu zao kwa kupaza sauti juu ya utunzanji wa Mazingira na kuacha kukata miti hovyo pamoja na kutumia Nishati safi ya kupikia ili kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia nchi ambayo yameleta madhara makubwa hapa nchini.
Ujumbe Siku ya Familia.

Akizungumzia siku ya Familia duniani,ametumia fursa hiyo kuwataka wazazi mkoani humo kuishi kwa upendo na kuacha migogoro ya kifamilia,ambayo imekuwa ikisababisha ukatili dhidi ya watoto na hata kusabisha tatizo la watoto wa Mitaani, huku akiwaomba viongozi wa dini kusaidia pia matatizo ya ndoa.

Kazi

Amewataka waandishi wa habari mkoani humo, kuandika habari za kuhamasisha wananchi wasichagua kazi, bali wafanye kazi yoyote ambayo itawasaidia kujipatia kipato na kuendesha maisha hao.
Mwenyekiti Shinyanga Press Club.

Mwenyekiti Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru, awali akisoma taarifa ya Klabu hiyo, amesema kwa taarifa iliyotolewa na Baraza la Habari Tanzania mwaka 2022 kwamba Mkoa wa Shinyanga umeshika nafasi ya Pili kwa Waandishi wa habari kufanyiwa madhira mbalimbali ikiwamo kunyimwa taarifa kutoka Ofisi za umma na binafsi.

Aidha, ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia kwa kufanya marekebisho ya sheria ya vifungu 9 ya sheria ya vyombo vya habari na kuongeza uhuru wa kujieleza, na sasa Tanzania inashika nafasi ya kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki, na kwa mujibu wa taarifa ya World Press Freedom kwa kushika nafasi ya 9 duniani.
“Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga sasa hivi tunatekeleza Mradi wa kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto wilayani Shinyanga, lakini kuna baadhi ya Watendaji wanawanyima taarifa waandishi wa habari, tunaomba hili Mkuu wa Mkoa ulitolee tamko ili kuwepo na uhuru wa habari hapa Shinyanga,”amesema Kakuru.

“Hivi karibuni Klabu yetu itakuwa na Mradi wa Uhuru wa kujieleza ambao utakutanisha wadau mbalimbali, na Mradi huu utawapa haki kwenu kama wadau kupaza sauti juu ya ustawi wa maendeleo ya Mkoa wetu,”ameongeza.
Kampeni ya Mazingira Shinyanga Press Club.

Ameomba wadau kushirikiana kikamilifu na Waandishi wa habari juu ya Kampeni ya utunzaji wa Mazingira ambapo Klabu hiyo hivi karibuni wanatarajia kufanya Kampeni ya utunzaji Mazingira yenye maudhui ‘Nafasi ya Vyombo vya Habari katika Mabadiliko ya Tabia nchi, kampeni ambayo itasaidia utekelezaji Mkakati wa Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia wa Mwaka 2024/2034.

Kauli Mbiu.

Kauli Mbiu ya Siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani Mwaka huu 2024 inasema “Uandishi wa Habari na Changamoto ya Mabadiliko ya Tabia Nchi”.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akiendelea kuzungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Mkoani humo.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari mkoani humo.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru akiendelea kuzungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari mkoani humo.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru akiendelea kuzungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari mkoani humo.
Meza kuu.
Maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Shinyanga yakiendelea.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akigawa Miche ya Miti kwenye Maadhimisho hayo ya Siku ya Uhuru wa vyombo vya habari mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akiendelea kugawa Miche ya Miti.

Picha ya pamoja ikipigwa.
Picha ya pamoja ikipigwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post