ALIYEOKOLEWA AKISOMBWA NA MAJI KWENYE MTO ATEMBEZEWA KICHAPO CHA MBWA MWIZI

                                      *** 

 Video ya mwanaume anayepigania maisha yake baada ya kujaribu kuvuka mto uliofurika kabla ya kuokolewa Jumanne, Aprili 30,2024 imepata hisia mseto kwenye mitandao ya kijamii.

Baada ya kuokolewa akizama alipata kipigo kutoka kwa mwokozi wake kwa kujaribu kuvuka mto bila kujali licha ya maji yaliyokuwa yakienda kasi. 

Video hiyo ilionyesha mwanaume huyo akimvuta hadi upande salama zaidi kabla ya kuanza kumpiga. 

Wale waliokuwa karibu walionekana kumshangilia jamaa huyo kwa kile watumiaji wa mtandao walisema kuwa ni ukumbusho. 


Wakenya walikuwa na maoni yapi kuhusu tukio hilo? 

Don alisema: "Huyo jamaa aliokolewa akisombwa na maji kisha akapewa kichapo cha mbwa kugharamia ukaidi wake, hapo sawa kabisa." 

Kijana wa baba alisema: "Wakenya hawajifunzi kamwe. Hakuna mtu anayepaswa kuvuka mito iliyofurika," 

Zachary Odongo alisema: "Sina tatizo na yeye kupigwa lakini kwanini aanzishe kipigo wakiwa bado mtoni. Adhabu ya papo hapo, kuwa fungo kwa wenye tabia kama hiyo,

Hatua hiyo inajiri baada ya Waziri wa Barabara na Uchukuzi Kipchumba Murkomen mnamo Jumatatu, Aprili 29 mjini Nakuru, kuwasihi Wakenya kuepuka kujihusisha na shughuli zinazohatarisha maisha.

 Murkomen alisema nini? 

Aidha aliwataka Wakenya kufuata sheria na maagizo ya serikali kuhusu hatua za usalama katika msimu huu. 

"Hebu sote tutii sheria na maagizo ya serikali usilazimishe njia yako usilazimishe madereva na magari ya umma kwa sababu tunataka watu wetu wawe hai. Wengi wa waliokufa ni kwa sababu ya ukaidi wao," Murkomen alisema. 

Murkomen alikuwa akizungumza huko Mai Mahiu Nakuru baada ya kuzuru eneo la Old Kijabe ambalo limegharimu maisha ya zaidi ya 70 kulingana na gavana wa Nakuru Susan Kihika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post