BABA AMZIKA MWANAE USIKU BILA JENEZA


Wakazi wa kijiji cha Nyaburu huko Gwasi nchini Kenya wamekosa amani baada ya kugunduliwa kwa kaburi la kina kirefu katika boma moja.

Mwanaume mwenye umri wa makamo, baba wa watoto watatu, aliripotiwa kumzika mwanawe wa miezi 5 kaburini bila jeneza, kufuatia kifo chake kinachodaiwa kuwa kutokana na ugonjwa usiku wa Alhamisi, Mei 16,2024. 

Majirani walioshuhudia tukio hilo waliogopa na wakatoa taarifa kwa viongozi wa eneo hilo. 

Naibu chifu wa eneo hilo Winnie Boit, akiandamana na maafisa kutoka kituo cha polisi cha Magunga, walithibitisha kisa hicho cha kutatanisha wakati wa ziara yao katika makazi ya mwanaume huyo, kulingana na Citizen Digital. 

Walieleza kuwa mwanaume huyo, alikuwa akiishi peke yake baada ya mkewe kurejea nyumbani kwa wazazi wake kwa matibabu ya kifafa, alikiri kitendo chake. 

Jamaa huyo amekamatwa na kwa sasa anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Magunga huku mamlaka ikiendelea na uchunguzi.

 Wakati huo huo, mwili wa mtoto huyo umepangwa kufukuliwa Jumatatu, Mei 27, 2024 kulingana na amri ya mahakama, kwa uchunguzi wa maiti.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post