KIPINDUPINDU CHAIBUKA TENA KISHAPU-WANANCHI,WATENDAJI WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI

 

Mganga Mkuu Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Dkt. Bahati Joseph akitoa taarifa ya lishe kwenye baraza la robo ya tatu la madiwani la Halmashauri lililofanyika leo Mei,9,2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri  hiyo huku akielezea kuibuka na  ugonjwa wa Kipindupindu katika baadhi ya Kata.

Na Sumai Salum _ Kishapu

Kata tatu za  Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga zimekumbwa na ugonjwa wa mlipuko wa Kipindupindu ikiwa ni pamoja na  Kata ya Mwamashele,Mwakipoya na  Kata ya Mwataga kijiji cha Mwamagembe.

Akiwasilisha taarifa ya Lishe Mganga Mkuu Wilaya hiyo Dr.Bahati Joseph kwenye kikao cha Robo ya tatu leo Mei,9 2024 lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo  amesema mpaka Mei,8 walikuwa jumla ya wagonjwa 13 waliolazwa katika kituo maalumu kilichotengwa kituo cha afya Kishapu.

"Tarehe 8 tulikuwa na wagonjwa ishirini na tisa (29) baadae wakaruhusiwa wakabakia 16 na usiku wa leo wameongezeka wagonjwa 2 na hapo baadae tunataraji kuwaruhusu baadhi wanaoendelea vizuri" amesema Dr. Joseph.

Aidha ameongeza kwa kutoa kanuni za kufuata ili kujikinga na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kunywa maji yaliyotibiwa au  yaliyochemshwa,kula chakula cha moto,kuzingatia usafi na matumizi sahihi ya vyoo na kunawa mikono kwa maji tiririka na safi.

Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Willium Jijimya amewaagiza Mganga Mkuu na wasimamizi wote watenge bajeti ya kuwezesha utoaji elimu ya kujikinga katika maeneo yaliyoathirika na ugonjwa huo.  
Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga wakifuatilia Kikao cha robo ya tatu cha baraza la madiwani kilichofanyika leo Mei,9,2024 katika ukumbi wa mikutano ya Halmashaur hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Willium Jijimya akizungumza kwenye baraza la madiwani la robo ya tatu leo Mei,9,2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
Afisa Maadili Kanda ya Magharibi Kutokea Tabora Bi.Halima Mnenge  akizungumza kwenye kikao cha robo ya tatu cha baraza la madiwani Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga kilichofanyika leo Mei,9,2024 katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo
Afisa Maadili kutoka Sekretarieti ya maadili Kanda ya Magharibi Tabora Bw. Vupala Mbillo akiwasilisha mada ya Uwajibikaji wa pamoja ikiwa ni miongoni mwa watoa elimu masuala ya maadili kwenye kikao cha robo ya tatu cha baraza la madiwani Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga kilichofanyika leo Mei,9,2024 katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post