WATU WAZIMA 6,238 WAFUNDISHWA KUSOMA , KUANDIKA NA KUHESABU KATIKA MIKOA 26

 

Serikali imefanikiwa kusajili wanafunzi 22,131 wakiwemo wasichana 2,794 wa elimu ya sekondari kwa njia mbadala katika vituo vya elimu ya watu Wazima pamoja na kutoa mafunzo ya kisomo kuimarisha stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kwa watu wazima 6,238 katika mikoa 26.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara hiyo kwa mwaka 2024/25ambapo amesema kuwa Serikali imekamilisha moduli 11 za hatua ya I na ll kwa ajili ya vituo 151 vya elimu ya sekondari kwa njia mbadala ili kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji katika vituo hivyo.

 Aidha imeongeza idadi ya vituo vya elimu ya sekondari kwa njia mbadala kutoka 168 hadi kufikia 190 kwa lengo la kuongeza fursa kwa wanafunzi waliokosa elimu kwa sababu mbalimbali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post