WIZARA YA AFYA KUWAKINGA WASICHANA DHIDI YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI

 


Na Dotto Kwilasa, DODOMA.. 

Wizara ya Afya, kwa kushirikiana na wadau wa
maendeleo imeandaa kampeni ya kitaifa ya kutoa,Chanjo ya Kukinga saratani ya mlango wa Kizazi kwa wasichana wote
walio na umri wa miaka 9 hadi 14 ili kukinga saratani ya shingo ya mlango wa kizazi . 

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Kinga, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma , Dkt.Tumaini Haonga ameeleza hayo  jijini Dodoma wakati wa
Mafunzo ya chanjo kwa waandishi wa habari yaliyoandaliwa  kuwawezesha  kůwa na uelewa sahihi kuhusu Kampeni hii. 

Akizungumzia ufanisi wa chanjo hiyo ameeleza kuwa ni dhabiti hata kama ikitolewa kwa dozi moja na kumfabya mhusika kuwa imara kwa vigezo vya shirika la afya duniani na kwamba   Ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi kama ilivyo kwa saratani nyingine sio rahisi kuona hatua za mwanzo licha ya kwamba una maambukizi. 

Naye Afisa Mpango wa Taifa wa chanjo Lotalis Norbert Gadau ameeleza kuwa asilimia 70 ya wanaofika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya huwa  wamechekewa huku wakiwa kwenye hatua mbaya  hadi kupelekea vifo.

Kutokana na hayo amewahimiza wasichana na wanawake kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara ili kukabiliana na saratani hiyo hali itakayisaidia  kupunguza na kuzuia viwango vya vifo vya wanawake, na kuleta matokeo Bora ya matibabu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post