VIONGOZI WA JUMUIYA YA MARIDHIANO NA AMANI KATA YA ISAKA WATAKIWA KUWA NA UONGOZI ULIOTUKUKA


Na Neema Nkumbi

Mkurugenzi idara ya ulinzi, usalama uwajibikaji na itifaki mheshimiwa Peter Kitanwa amewataka viongozi wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Kata ya Isaka Wilayani Kahama kuwa na uwajibikaji uliotukuka baada ya kusimikwa rasmi kuwa viongozi katika Kata hiyo.

Peter Kitanwa amesema hayo katika hafla ya kuwasimika viongozi hao iliyofanyika april 17, 2024 ambapo viongozi waliosimikwa ni ngazi ya mwenyekiti, makamu mwenyekiti, katibu, makamu katibu muhasibu , mzee wa mila pamoja na wajumbe


''Mmeazimwa hiyo dhamana na moja ya majukumu yangu nikufuatilia utendaji mpaka ngazi ya kata kwa sasa tutatoa macho zaidi kuona kama kuna matokeo tunayoyatarajia, lazima muwe na vikao vya mara kwa mara kwa kuwa hakuna kazi ya mtu mmoja hivyo jitahidini kuwajibika vizuri ili mpate kufanikiwa'' ,amesema Peter Kitanwa


Naye mwenyekiti mteule Shaban Twaha akizungumza kwa niaba ya viongozi wenzake amesema kuwa wao ni watoto waliozaliwa na kutembea hapo hapo pia ameahidi ushirikiano kwaanzia wao kwa wao kwenye Kata, Wilaya hata Taifa

''Wananchi tutumeni nasi tutafanya pia tushaurini tutashaurika maana kiongozi mzuri ni yule anaeshaurika hivyo ninachowaahidi wananchi wa isaka ni kuitendea kazi nafasi hii na kuwa jumuisha wananchi wa isaka ili wajie chombo hiki ni chombo gani, ni kweli isaka kuna migogoro mingi ila nina imani kuwa tutawapatanisha na kuwa na amani hivyo tunaomba ushurikiano kutoka kwa wananchi'', amesema Shaban.

Pia wananchi wa Kata ya Isaka Azaki Mwamudu na Abdala jumanne wamefurahi kupata jumuiya hiyo katika kata yao, na wanaamini kuwa itawasaidia kutatua migogoro iliyopo katika kata hiyo badala ya kupelekana mahakamani hivyo tumepata sehemu ya kukimbilia

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post