TRA YAHAMASISHA WAENDESHA BODABODA KULIPA KODI





Na Mbuke Shilagi Bukoba

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imewataka wafanyabiashara wa bodaboda kulipa kodi kwa mwaka Tsh. 65,000/= ambapo kodi ya TRA inalipwa kwa awamu nne sawa na Tsh. 16200/= kwa miezi mitatu.

Akizungumza katika kikao cha mafunzo ya elimu ya kodi na waandishi wa habari Aprili 25,2024 katika ukumbi wa mkutano wa ofisi ya meneja TRA Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Meneja wa TRA Mkoa wa Kagera Bw. Castro Johm amesema kuwa kupitia mabadiliko ya sheria ya mwezi Julai 2023 wafanyabiashara wote wa bodaboda wanatakiwa kulipa kodi.

Aidha,  John amesema kuwa wafanyabiashara wote wa bodaboda ambao hawajafanyiwa makadirio waende ofisi za TRA kufanyiwa makadilio na kwamba kutolipa kodi ni kinyume na sheria na kuna penalti ambayo inaweza kuwakumba na kwamba ambaye atakuwa anahitaji ufafanuzi au ana mkwamo wowote afike ili kutatuliwa changamoto yake.

 Kodi yoyote unapolipa mapato unapata stika ya mapato ambayo unaenda kubandika kwenye chombo chako kulingana na umelipa ya mwaka  au miezi mitatu unapata kulingana na stika na kunasitika zinazotofautisha kama umelipa au hujalipa'', amesema.

Sambamba na hayo Bw. John ametoa wito kwa watu wote walio uza au kuuziwa chombo cha moto kufika ofisini ili kubadilisha jina na kwamba utaratibu ni rahisi ambapo ataenda na mkataba pamoja na EFD LIST ili kubadilisha uhamisho wa chombo hicho.

Kama mnavyojua kutobadilisha umiliki kunamadhara mengi kwamfano kumekuwa na kesi chombo cha moto kinatumika kwenye matukio ya uhalifu mfano chombo cha moto kinajina la Castro pengine itajulikana wewe umefanya uhalifu  lakini unakuta uliuza muda mrefu kwahiyo kubadilisha jina mbali na kuwa na uhalali nacho ila pia inakuepusha na mambo kama hayo'', amesema Bw. John

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post