TAASISI YA INTERNET SOCIETY YAJA NA SULUHISHO LA GHARAMA ZA BANDO

Taasisi ya Internet Society Tanzania imewahimiza wananchi kutumia fursa ya huduma ya Internet kujiletea maendeleo, badala ya kufuatilia mambo yasiyo ya msingi na kupoteza muda na gharama za bando.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Nasar Kirama wakati akitoa semina kwa wadau wa Internet wakiwemo waalimu, viongozi wa dini, viongozi wa serikali za mitaa, wajasiriamali na mashirika yasiyo ya serikali katika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.

Kirama alisema huduma ya Internet ikitumika vyema inaweza kubadili maisha ya wananchi ikizingatiwa mwelekeo uliopo sasa ni uchumi wa kidijitali na hivyo kuwahimiza wananchi kutumia fursa hiyo kimaendeleo.

Hata hivyo Kirama alisema baadhi ya maeneo hususani ya pembezoni huduma ya Internet haijawafikia wananchi huku waliofikiwa na huduma hiyo wakitatizwa na gharama za bando na hivyo kueleza kuwa taasisi yake imekuja na suluhisho ambapo wanajamii sasa wanaweza kuungana pamoja na kuchangia upatikanaji wa Internet yenye kasi na kwa gharama nafuu.

Alisema tayari majaribio ya huduma ya wananchi kuchangia Internet (Communit Network) yameleta mafanikio makubwa katika wilaya ya Kigamboni jijini Dar es salaam na hivyo kutoa rai kwa wakazi wa Mwanza kuichangamkia.

Mmoja wa mdau wa Internet ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la MIBOS, Hassan Rangi alisema miundombinu ya mfano iliyofungwa na taasisi ya Internet Society Tanzania katika shirika hilo imesaidia upatikanaji wa huduma ya uhakika na kwa gharama nafuu.

Naye Mratibu wa shirika la GWEITA, Hadija Ferooz alisema huduma ya mtandao wa jamii (Community Network), itasaidia jamii kupata uhakika wa internet na kuondokana na matumizi makubwa ya gharama za bando.
Na George Binagi- GB Pazzo, Mwanza
Wadau wa mtandao wa Internet wakiwemo waalimu, viongozi wa Serikali za Mitaa, wajasiriamali na mashirika yasiyo ya kiserikali katika Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza wakijifunza kuhusu Mtandao wa Jamii (Community Network) iliyofungwa katika ofisi za shirika la MIBOS zilizopo Kiloleli wilayani Ilemela.
Mkurugenzi wa taasisi ya Internet Society Tanzania, Nasar Kirama (kulia) akiwasilisha mada kwa wadau wilayani Ilemela mkoani Mwanza kuhusu Mtandao wa Jamii (Community Network) unaotoa fursa kwa wanajamii kuungana pamoja na kuchangia upatikanaji wa huduma ya Internet yenye kasi na kwa gharama nafuu.
Wadau wa Internet wilayani Ilemela wakifuatilia mada wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kuhusu Mtandao wa Jamii (Communituy Networt) iliyotolewa na taasisi ya Internet Society Tanzania yenye makao yake makuu jijini Dar es salaam.
Wadau wa Internet wilayani Ilemela wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kujengewa uelewa kuhusu Mtandao wa Jamii (Communituy Networt) na taasisi ya Internet Society Tanzania.
Tazama Video hapa chini
SOMA PIA>>> HABARI ZAIDI HAPA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post