STANBIC BANK NA RAMANI KUWAPA MIKOPO WASAMBAZAJI WA BIDHAA ZA VIWANDANI


Mkurugenzi wa biashara wa Benki ya Stanbic Frederick Max na Afisa Mkuu Mtendaji wa Ramani (Mkurugenzi Mtendaji), Lain Usiri, wakipeana mikono Mara baada ya kusaini Makubaliano jijini Dar es salaam.

********

BENKI ya stanbic imeingia Makubaliano na Kampuni ya ramani kwa lengo la kuwafikia Wafanyabiashara wanaosambaza bidhaa mbalimbali za viwandani kwa kuwapa mikopo na mitaji ya kuendeleza biashara zao.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana wakati wa kuingia Makubaliano hayo Mkurugenzi wa biashara wa Benki hiyo Frederick Max ameeleza kuwa Makubaliano hayo yataiwezesha Benki hiyo kufikisha Huduma za kibenki kwa wateja wengi Zaidi.

Amebainisha kuwa Benki imeshatoa mikopo yenye thamani ya bilioni 50 kwa Mwaka Jana ambapo kwa Mwaka huu ikitarajia kutoa shilingi bilioni 150 kwa ajili ya wasambazaji wa bidhaa za viwandani.

"leo tumeingia makubaliano na ramani ili kuweza kuwafikia wasambazaji wa bidhaa mbalimbali hii itatuwezesha sisi kufikisha huduma zetu za kibenki kwa wahitaji wengi zaidi kwasababu ramani tayari wanawateja wao nchi nzima na sisi tunaleta ujuzi wetu wa masuala ya kibiashara"

"Sisi kama Benki tunajiskia fahari na faraja kuweza kuwa nao kuhakikisha wafanyabiashara wengi sana wanafaidika na huduma za kibenki

Kiasi ambacho tumetenga sisi kwaajili ya uwezeshaji ni tayari tumetoa mikopo yenye hamani ya Bilioni 50 kuanzia Desemba mwaka 2023 Hadi sasa na mwaka huu tunatarajia ‘kuongeza hiyo namba maradufu" Alisema Max

Kwa upande wake Afisa Mkuu Mtendaji wa Ramani (Mkurugenzi Mtendaji), Iain Usiri, alisema kuwa Makubaliano hayo yataiwezesha Benki hiyo kuwafatilia wateja wao kwa ukaribu zaidi lakini pia yamelenga kufikisha ujumuishi wa Huduma kifedha kwa watanzania.

Pia alisema kampuni hiyo inawapa wauzaji programu ya teknolojia ya umiliki wa kifedha ili kurahisisha shughuli zao.

"Kwa hivyo tunazindua soko la fedha ili benki inayofanya kazi nasi kupitia teknolojia yetu iweze kupata data ya wakati halisi na tathmini za hatari za wauzaji wa FMCG"

Akiongeza "Kabla ya teknolojia hii, benki hazina mwonekano wa mauzo ya wauzaji wa FMCG, hii itawezesha taasisi za kifedha kupata data ya wakati halisi na tathmini za hatari."

Aliongeza kuwa hatua hiyo inakwenda kukuza biashara ya ndani nchini na ushirikishwaji wa kifedha


Mkurugenzi wa biashara wa Benki ya Stanbic Frederick Max akisaini Makubaliano na Kampuni ya Ramani jijini Dar es salaam April 22,2024.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Ramani (Mkurugenzi Mtendaji), Iain Usiri, akisaini Makubaliano na Kampuni ya ramani jijini Dar es salaam April 22,2024.

Picha ya pamoja ya viongozi wa Ramani na Benki ya Stanbic katika hafla fupi ya kusaini Makubaliano hayo.




Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya makubaliano kati ya Kampuni ya ramani na banki ya Stanbic Bank yenye lengo la kuwafikia Wafanyabiashara wanaosambaza bidhaa mbalimbali za viwandani kwa kuwapa mikopo na mitaji ya kuendeleza biashara zao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post