MAMA, MTOTO WAKATWA MAPANGA NA MUME ALIYELEWA


Mwanamke anayefahamika kwa jina Rhobi Mwita Nkori mkazi wa Serengeti mkoani Mara amenusurika kuuawa kwa kukatwa mapanga na mume wake ambaye alidaiwa kurudi nyumbani akiwa amelewa na kuanza kufanya vurugu.


EATV imezungumza na Rhobi Mwita Nkori ambaye, mwathirika wa tukio hilo ambaye amesema kuwa mume wake anayefahamika kama Wansato Marwa alirudi nyumbani akiwa amelewa na kuchukua panga na kuanza kumkata sehemu mbalimbali za mwili wake na alivyofanikiwa kumtoroka ndipo akamkata panga mwanae wa kike mwenye umri wa miaka 10 katika sehemu ya kichwa.

Naye, msamaria mwema aliyempokea mwanamke huyo baada ya kufika wilayani Tarime, Suzana Mkami Marwa ameleza kuwa mwanamke huyo alifika nyumbani kwake akiwa na watoto 6 mmoja akiwa amekatwa mapanga pamoja na mama yake huku akiiomba serikali kumchukulia hatua kali za kisheria aliyehusika na tukio hilo.

CHANZO - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post