INLAND RADIO YAANZISHA TIMU YA MPIRA WA MIGUU "INLAND FOOTBALL CLUB"

 

Kutokana na umuhimu w kujali vipaji vya wanamichezo wachanga, Inland Radio kupitia kipindi chake cha Michezo kiitwacho #BungeLaMichezo ambacho kinaruka kila Jumatatu hadi Jumapili kimefanya usaili na timu ya kuanzisha timu yake inayoitwa #InlandFootballClub.

Zoezi la usaili wa wachezaji hao watakaounda timu hiyo umefanyika leo 27 April 2024 katika Uwanja wa Kanisa la Baptist lililopo Kona ya Bwiru Kata ya Nyamanoro Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.


Jumla ya Wachezaji Kumi na tano wamechaguliwa kutengeneza kikosi hicho ambacho kitaanza kucheza mechi mbalimbali za Kirafiki ili kuleta ushirikiano ya Radio yetu na Jamii kwa ujumla ambayo ndio wateja wa vipindi vyetu hewani.


Vigezo vya usaili huo ulikuwa kuchukua Fomu kisha kuijaza kwa mhusika kuirudisha. Pia suala la umri limezingatiwa kwa wachezaji hao maana hata Shirikisho la Soka Tanzania limetoa maelekezo kuandaa timu kwa umri usiozidi miaka 20.


Baada ya usaili kukamilika sasa linafuata zoezi la mazoezi ya kuandaa timu. Mazoezi hayo yanatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Shule ya Sekondari Kitangili iliyoko Bwiru Mwanza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post