BAWACHA YAHAMASISHA WANAWAKE KUJITOKEZA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI



Na Mbuke Shilagi Bukoba.

Mwenyekiti wa baraza la wanawake Chadema (BAWACHA) Mkoa wa Kagera Bi. Magrethi Kyai amezungumza na wanawake  wa Chadema pia baraza la wanawake chadema Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera kujitokeza na kugombea katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

 
Akizungumza na Baraza la Chadema Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Aprili 17,2024 akiwa na ajenda tatu ambazo ni ujenzi wa chama, chaguzi za serikali za mitaa na kutembea kila kata ili kuwajenga wanawake kujiamini na kujifahamu na kugombea ambacho kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Bawacha wilaya kata pamoja na mitaa, amesema kuwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa wanawake lazima wajitokeze kugombea katika nyadhifa zote.

"Hatukuja ili kuishia hapa ila kila mwanamke tutahakikisha kwamba anaenda kugombea na kujielezea na kusimama kisiasa na kujua wajibu wake kisiasa na kiuchumi",amesema Magreth.

"Na tutafanya semina ili kumjenga mwanamke na kilichotuleta zaidi ni kuongea na nyie tujue kuwa Manispaa ya Bukoba kunatakiwa nini na tuanzie wapi na tusimame vipi lakini nawashukuru sana wanachama Kutoka kata zote" ,amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post