ASKOFU ACHOMWA AKIHUBIRI KANISANI


Askofu Mar Mari Emmanuel

Askofu mmoja wa Kanisa la Christ the Good Shepherd Church jijini Sydney huo Australia ambaye vyombo vya habari vya nchi hiyo vimemtaja kwa jina Mar Mari Emmanuel amedungwa kitu chenye ncha kali mithili ya kisu wakati akitoa mahubiri kwa waumini wake.

Polisi nchini humo wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba tayari mshukiwa amekamatwa baada ya kufanya tukio hilo la kumjeruhi askofu Mar Mari Emmanuel ambaye kwa mujibu wa taarifa ya polisi hakupata majeraha makubwa ya kuhatarisha uhai wake.

Video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii inamuonyesha mtu aliyevaa mavazi meusi akimsogelea askofu huyo na kuanza kumshambulia wakati akitoa mahubiri.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post