Na Mwandishi wetu, RWANDA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) amekutana na Waziri wa Nchi Kilimo na Mifugo wa Rwanda kujadili na kuweka sawa mikakati ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata maziwa jijini Mwanza.
Tanzania ni nchi ya tatu kwa kuwa na mifugo mingi zaidi Afrika, wafugaji wa Tanzania wanahimizwa kufuga mifugo ya kisasa na kuzalisha maziwa kwa wingi ili kukidhi mahitaji ya kiwanda hicho.
Mjadala huo umejumuisha wawakilishi kutoka Wizara ya Kilimo pamoja na Bodi ya Maziwa, Bw. Gungu Mibavu na Prof. George Msalya, mtawalia.
Aidha, katika majadiliano hayo viongozi hao wawili wamejadili kuboresha na kuongeza uzalishaji wa nafaka kwa Watanzania na kuongeza uingizaji wa bidhaa hizo nchini Rwanda ambapo katika bidhaa za chakula huagiza mchele mwingi kutoka Tanzania.
Hati ya Makubaliano ya kujengwa kwa kiwanda hicho cha maziwa Mwanza ilisainiwa Januari mwaka huu kati ya Tanzania na wawekezaji wa Rwanda.