RAIS TCCIA ASHANGAZWA NA UWEKEZAJI MKUBWA KIWANDA CHA JAMBO

Rais wa Chemba ya Biashara Viwanda na kilimo Tanzania (TCCIA) Vicent Bruno Minja amefanya ziara ya kutembelea kiwanda cha Jambo Food Products kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga kuangalia shughuli za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa katika kiwanda hicho.

Minja amefanya ziara hiyo leo Ijumaa Machi 8,2024 , akiwa ameambatana na Wajumbe wa TCCIA mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili wawekezaji ili aweze kuzifikisha ngazi husika ili ziweze kupatiwa ufumbuzi

Aidha Minja ameonyesha kushangazwa na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Salum Hamis katika mkoa wa Shinyanga na kuahidi kutoa ushirikiano kwa uongozi wa kiwanda hicho kutatua changamoto zinaz changia kukwama kwa uzalishaji katika kiwanda hicho.

Kwa upande wake Mmiliki wa kiwanda cha Jambo Food Products Salum Hamis, amemshukuru Rais wa TCCIA kwa kufanya ziara katika kiwanda hicho na kumuomba kuendelea kutatua kero zinazowakabili wafanya biashara hali itakayosaidia wafanya biashara hao kukua kiuchumi.






Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post