BUKOBA MJINI MPYA YAIGUSA JAMII YA MUSIRA KATIKA UJENZI WA MSIKITI, WAGAWA MAJIKO YA GESI

Wanakamati kutoka group la Whatsapp la Bukoba Mjini Mpya wakikabidhi saruji kwa kiongozi wa msikiti wa Musira
Na Mariam Kagenda _  Kagera

 Wadau wa group la Whatsapp lijulikanalo kama  Bukoba Mjini mpya kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini  ambaye pia ni  Naibu Waziri wa mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Stephen Byabato  wametoa msaada wa saruji mifuko 20 kwa ajili ya ujenzi wa msikiti  pamoja na mitungi 15 ya gesi kwa mama lishe katika kisiwa cha Musira kilichopo kata ya Miembeni  Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.


Wakati akipokea misaada hiyo Diwani wa kata ya Miembeni Richard Gaspar kwa niaba ya wananchi wa kisiwa cha Musira amewashukuru wadau wa group hilo pamoja na mbunge wa Jimbo la Bukoba  kwa kuikumbuka jamii ya Musira kwani Saruji hiyo itasaidia katika ujenzi wa Msikiti wa waumini wa dini ya kiislamu kwenye kisiwa hicho na mitungi ya gesi itawasaidia mama lishe kurahisisha shughuli zao kwani walikuwa wanapata shida kupata mkaa hasa kipindi cha mvua.

Naye mmoja wa wanakamati walioratibu shughuli ya misaada hiyo kutoka   Group la Whatsapp la Bukoba Mjini Mpya, Jamila Emily  amesema kuwa ikiwa ni mwendelezo wa group hilo kuigusa jamii ya wana Bukoba mjini waliona katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani waguse kwa wananchi wa  kisiwa cha Musira kwa kutoa Saruji ya kuwezesha ujenzi wa msikiti ili wananchi wa kisiwa cha Musira waweze kuswalia sehemu salama .

 Emily amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini Stephen byabato pamoja na wadau wa maendeleo kutoka group la Bukoba mjini mpya  na wanakamati walioratibu  swala hilo kwa kuona umuhimu wa jambo hilo na kutoa michango ya kufanikisha kupatikana misaada iliyotolewa.

Naye mwenyekiti wa Msikiti wa Musira Yakub Fresh amesema kuwa msaada huo utasaidia kutatua changamoto iliyopo kwani kwa sasa wanaswalia katika kibanda  cha mtu sehemu ambayo sio salama  ambapo   baada ya uwepo wa changamoto hiyo waliamua kuanzisha ujenzi wa msikiti ambao umefikia hatua ya madirisha hivyo Saruji hiyo itasaidia kupiga hatua kubwa ya ujenzi wa Msikiti ili waweze kupata msikiti wa kuswalia 

Nao Mama lishe waliopokea majiko ya gesi wamesema kuwa sasa kisiwa cha Musira kinaenda kuwa kisiwa cha mfano kwa utumiaji wa nishati salama .wameshukuru kuletewa msaada wa gesi na kusema kuwa  wateja wao watakuwa wakipata chakula cha moto wakati wote kwani hapo awali walikuwa wanapata changamoto ya mkaa kuutoa nchi kavu kuuleta katika kisiwa hicho wakati mwingine ulikuwa unafika ukiwa umeshalowa na maji hivyo kwa sasa hawatoangaika tena na mkaa jambo ambalo litasaidia wateja wao kupata huduma  nzuri ya chakula wakati wote.

Wanakamati walioratibu msaada wa Musira

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post