CCM YAJAZA NAFASI ZILIZO WAZI MOROGORO


Na Christina Cosmas, Morogoro

HALMASHAURI kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro 
imemteua na kumpitisha Gervas Mbaruku Zugumbwa kugombea nafasi ya udiwani kwenye uchaguzi mdogo ndani ya kata ya Kamwene wilayani Kilombero.

Akizungumza kupitia taarifa yake kwa vyombo vya Habari Katibu wa siasa, Uenezi na mafunzo mkoani hapa Zangina Shanang Zangina alisema CCM kupitia kikao cha kawaida cha Mkoa wa Morogoro chini ya mwenyekiti Mhandisi Joseph Masunga kimefanya uteuzi na kuwapitisha wagombea mbalimbali wa kujaza nafasi mbalimbali zilizokuwa wazi katika chama.

Zangina alisema katika nafasi ya mwenyekiti wa CCM kata ya Konde Wilaya ya Morogoro Vijijini waliopitishwa ni wagombea watatu ambao ni pamoja na Augustina Lucas Makonde, Salum Shaban na Nestory P. Mbena.

Alisema nafasi ya ukatibu wa CCM kata ya Bungu Wilayani Morogoro Vijijini waliopitishwa pia ni wagombea watatu ambao ni Abdalah A. Lubegete, Athumani Shomari Hega na Hashimu Omari Shabani.

Zangina alisema pia nafasi ya ukatibu wa CCM kata ya Kalengakelu Wilayani Kilombero waliopitishwa ni Anthony Mwangwela, Frank Lyanzile na Vicent Mkanyipelele.

Alitaja nafasi nyingine iliyopata wagombea kupitishwa kuwa ni ya uenyekiti wa CCM kata ya Mkula Wilayani Kilombero ambapo aliwataja wagombea waliopitishwa kuwa ni Athuman J. Molem, JunisiaP. Mtangire na Robert V. Njogope.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments