ASKARI WANANDOA WALIOFARIKI KWA AJALI WAOMBEWA KWA KUFANYIWA IBADA

 


Na Mwandishi Maalum Jeshi la Polisi- Arusha.

Mtandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Arusha TPF-Net katika kuelekea siku ya wanawake Duniani leo wamefanya ibada maalumu kwa ajili ya kuwaombea Askari Polisi wanandoa waliofariki Dunia kwa ajali ya gari siku mbili baada ya kufunga ndoa.

Akiongea mara baada ya ibada hiyo iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Theresia Jijini Arusha Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoani humo Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Happiness Temu amesema mtandao huo umekuwa na utaratibu wa kuyakumbuka makundi mbalimbali yenye uhitaji katika jamii ambapo kwa mwaka huu waliona ni vyema kuwakumbuka Askari waliofariki kwa ajali.

ASP Temu amebainisha kuwa wameamua kufanya Ibada hiyo ikiwa ni sehemu ya kuwaombea marehemu hao ambao walikua wanafanya nao kazi Mkoani humo kabla kupatwa na umauti Disemba 20, 2022 ambapo pia katika ibada hiyo wamewaombea Watoto wawili ambao waliachwa na marehemu.

Nao baadhi ya askari wa mtaandao huo waliofanya kazi kwa Karibu na marehemu wamebainisha Pamoja na kuwaombea marehemu, pia wametumia ibada hiyo kumshukuru Mungu kwa kuendelea kuwalinda katika utekelezaji wa majukumu yao.

Kwa upande wake Mrakibu wa Polisi SP Asia Matauka ambaye anafanya kazi katika Mkoa wa Kilimanjaro amesema mara baada kusikia juu ya uwepo wa ibada hiyo aliona ni vyema kuungana na mtaandao huo kuwaombea marehemu.

Askari waliofariki na kufanyiwa ibada leo ni Konstebo Noah Simfukwe na Agness Martin. 
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments