Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akizungumza kwenye mkutano mkuu wa 29 wa SHIRECU
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkutano Mkuu wa 29 wa Chama cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) umebariki maamuzi ya Bodi ya SHIRECU kuhusu uamuzi wa kumsimamisha ujumbe wa Bodi Mwenyekiti wa Bodi ya SHIRECU Kwiyolecha Nkilijiwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka na unyanyasaji wa watumishi na ubabe katika uendeshaji vikao na kutosikiliza ushauri wa wajumbe.
Katika Mkutano huo uliofanyika leo Jumanne Machi 26,2024 katika ukumbi wa SHIRECU ukiongozwa na Mwenyekiti wa mkutano huo, Yohana Maganga, ambapo wajumbe 115 wameunga mkono maamuzi ya Bodi ya SHIRECU kumsimamisha uongozi bwana Kwiyolecha Nkilijiwa na hakuna mjumbe aliyepinga maamuzi hayo.
Awali Makamu mwenyekiti wa SHIRECU Josephat Limbe ametoa taarifa ya SHIRECU akielezea changamoto za kiungozi na usimamizi wa Chama ambapo amesema mnamo Mei 5,2023 bodi ya SHIRECU ilichukua uamuzi wa kumsimamisha ujumbe wa bodi Mwenyekiti wa Bodi hiyo,Kwiyolecha Nkilijiwa kutokana na sababu mbalimbali.
Amezitaja sababu hizo kuwa ni Matumizi mabaya ya madaraka na unyanyasaji wa watumishi ambapo mwenyekiti huyo alikuwa na tabia ya kunyanyasa watumishi wasiotekeleza maelekezo yake yasiyo sahihi kwa kwenda kinyume na kanuni za utendaji kazi akisingizia hamisho hizo ziliamuliwa na Bodi wakati si kweli.
“Kwa mfano alimhamisha Kaimu Mhasibu Mkuu mwenye Diploma ya Uhasibu bi. Rachel Mahona na kumpeleka Mhunze kuwa Karani wa fedha na kumleta bi Selina Matembe asiyekuwa na taaluma yoyote ya fedha kuja kuwa Mhasibu Mkuu akisingizia kuwa kikao cha bodi cha Tarehe 4/11/2021 kilifanya maamuzi hayo wakati tarehe tajwa hakukuwa na kikao chochote cha Bodi. Kitendo cha kumleta bi. Selina Matembe ilitoa fursa kwa mwenyekiti wetu kumwelekeza afanye malipo pasipo kuzingatia kanuni za fedha likiwemo lile la Shilingi 3,800,000/= na shilingi 500,000/= kwenda kwa Mrajis Msaidizi eti kwa lengo la kumnyamazisha ili asichukue hatua ya kurejeshwa kwa hizo Shilingi 3,800,000/= jambo ambalo Mrajis alilitafsiri ni hongo”,ameeleza Makamu mwenyekiti huyo.
Ameitaja sababu nyingine ni Ubabe katika uendeshaji wa vikao na kutosikiliza ushauri wa wajumbe wa Bodi akitolea mfano kuwa, Mkutano Mkuu wa 28 uliagiza dengu zilizonunuliwa ziuzwe haraka ili kupunguza hasara isiwe kubwa, bodi ilipoketi kutaka kutekeleza agizo hilo la mkutano mkuu, Mwenyekiti huyo alikataa na kudai wasubiri atafute mnunuzi mzuri kitu kilichopelekea dengu hizo zibunguliwe na hivyo kupelekea baadae ziuzwe kwa bei ya chini shilingi 600/= kwa kilo badala ya sh. 1150/= hivyo kupelekea chama kipate hasara ya shilingi 550/= kwa kila kilo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya SHIRECU Kwiyolecha Nkilijiwa akijieleza kwenye mkutano mkuu wa 29 wa SHIRECU
“Sababu nyingine ni ajira ya kibabe ya Meneja Mkuu, ambapo chama chetu kiliajiri Kaimu Meneja Mkuu kinyume cha sheria ya vyama vya ushirika ya namna ya kuajiri watendaji wakuu wa vyama vya ushirika (Meneja Mkuu, Mhasibu Mkuu na Mkaguzi wa ndani),ambapo sharia inataka watendaji hao lazima nafasi zao zitangazwe na watakaojitokeza kuziomba sharti wafanyiwe upekuzi na Mrajis wa vyama vya Ushirika au mtu yeyote atakayemtaka kutekeleza jukumu hilo”,ameeleza.
“Ajira hii alipoileta Mwenyekiti, bodi n ahata aliposhauriwa kwa kusomewa kifungu cha sharia ya ushirika juu ya ajira hizo bw. Kwiyolecha Nkilijiwa alikaidi, jambo hili lilipelekea aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya ajira, nidhamu, elimu na mafunzo ndugu Charles Jishuli ajiuzulu nafasi hiyo kwa lengo la kupinga ubabe wa mwenyekiti”,ameongeza.
Hata hivyo,Kwiyolecha Nkilijiwa alipopewa nafasi ya kuzungumza kwenye mkutano huo amesema madai hayo siyo ya kweli na hajapewa nafasi ya kusikilizwa.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro amesema ni jukumu la Chama cha Ushirika kumtafutia mkulima soko la mazao yake huku akiahidi kusimamia Ushirika Shinyanga kwani lengo ni kuhakikisha mkulima ananufaika na ushirika.
“Moja ya ajenda zangu kama Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga ni kuhakikisha Ushirika unasimama vizuri Shinyanga, tunataka kujenga tija, ushirika ni kitu kikubwa sana, na ushirika duniani ni dudu kubwa, ukisimamia vizuri ushirika mtapata pesa nyingi…Mimi nitakuwa mlinzi wenu, nimekuja kuwasimamia mpate tija kwenye vyama vyenu”,amesema Mkuu wa Wilaya.
“Nina mamlaka ya kutosha ya kusimamia Ushirika, ninataka wakulima wa Shinyanga watendewe haki. Tuachane vya vyama vya Ushirika vya Kula na kulala, Shinyanga tusichezee ushirika, ushirika unakuza uchumi.
Mameneja na Wenyekiti wa vyama vya msingi nataka kujua Profile na mipango ya vyama vyenu, nataka chama kimoja kimoja ifikapo tarehe 10.4.2024..Kwa hiyo muende mkajipange tunataka kusaidia taifa hili”,amesema Mtatiro.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akizungumza kwenye mkutano mkuu wa 29 wa SHIRECU
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akizungumza kwenye mkutano mkuu wa 29 wa SHIRECU
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akizungumza kwenye mkutano mkuu wa 29 wa SHIRECU
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akizungumza kwenye mkutano mkuu wa 29 wa SHIRECU
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya SHIRECU Kwiyolecha Nkilijiwa akijieleza kwenye mkutano mkuu wa 29 wa SHIRECU
Makamu Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga SHIRECU (1984) Ltd, Josephat Limbe akizungumza leo Jumanne Machi 26,2024 wakati wa Mkutano Mkuu wa 29 wa SHIRECU
Makamu Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga SHIRECU (1984) Ltd, Josephat Limbe akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 29 wa SHIRECU
Mrajis Msaidizi wa Vyama vya ushirika Mkoa wa Shinyanga, Hilda Boniphace akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 29 wa SHIRECU
Mrajis Msaidizi wa Vyama vya ushirika Mkoa wa Shinyanga, Hilda Boniphace akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 29 wa SHIRECU
Mkutano Mkuu wa 29 wa SHIRECU ukiendelea
Mkutano Mkuu wa 29 wa SHIRECU ukiendelea
Mkutano Mkuu wa 29 wa SHIRECU ukiendelea
Mkutano Mkuu wa 29 wa SHIRECU ukiendelea