DKT. BITEKO AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI MKUBWA WA UZALISHAJI UMEME JUA KISHAPU - SHINYANGA, ATAKA UKAMILIKE KWA WAKATI

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Naibu Waziri  Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko ameitaka Kampuni ya Sinohydro Corporation Limited iliyopewa kandarasi ya kujenga Mradi uzalishaji Umeme wa Jua Megawati 150 wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 323 unaotekelezwa katika kijiji cha Ngunga kata ya Talaga Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kukamilisha ujenzi huo kwa wakati ndani ya muda waliokubaliana na bila kuongeza bajeti ili wananchi waanze kunufaika na huduma ya umeme.

Dkt. Biteko ametoa agizo hilo leo Alhamisi Machi 14,2024 wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi mradi wa uzalishaji umeme jua Megawati 150 iliyohudhuriwa na viongozi na wananchi mbalimbali.


"Huu ni mradi mkubwa sana wa umeme unaoshindana na mradi wa Kihansi. Nikuombe Mkandarasi Sinohydro Co. Ltd uliyepewa dhamana ya kujenga mradi huu mkubwa wa umeme nchini utekeleze ndani ya muda uliopangwa. Kukamilika kwa mradi huu kutasaidia kupunguza changamoto ya umeme nchini. Tunataka wananchi wapate huduma ya umeme wa uhakika", amesema Dkt. Biteko.
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko (katikati) akiweka jiwe la msingi Mradi uzalishaji Umeme wa Jua Megawati 150 Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga

Dkt. Biteko amesema mradi wa Umeme Jua utaanza kuzalisha megawati 50 ifikapo mwezi Januari mwaka 2025 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuongeza vyanzo vya umeme kwani vilivyopo bado havitoshelezi mahitaji ambapo lengo la Serikali ni kuibua, kuendeleza na kutekeleza vyanzo mbalimbali vya umeme ili kuondokana na utegemezi wa Maji na Gesi Asilia kuzalisha umeme.

“Vyanzo vingine vya umeme tunavyoviendeleza ni pamoja na mradi wa Jotoardhi Songwe na Mbeya ambapo tarehe 1 Aprili mwaka huu uchorongaji unaanza katika eneo la Ngozi, mradi mwingine unaoenda kutekelezwa ni mradi wa megawati 100 wa upepo uliopo Makambako ambapo fidia imeanza kulipwa”, amesema Dkt. Biteko.

Aidha ameishukuru Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) kwa kutoa fedha za kutekeleza mradi huo.

Katika hatua nyingine ameziagiza TANESCO na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kuhakikisha wanawapelekea wananchi huduma ya umeme kwa haraka na kama kuna changamoto ya umeme wananchi hao wapate taarifa mapema.

Hali Kadhalika Dkt. Biteko,  ameagiza Watendaji wa Serikali kuhakikisha kuwa wanaweka mitambo ya umeme Jua kwenye majengo yao ili kutokuwa tegemezi kwenye umeme wa gridi pekee na kusema kuwa Wizara ya Nishati na Taasisi zake zitaanza kutekeleza suala hilo.

Aidha amewataka Wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini ambao ni SUMA JKT (Wilaya ya Kishapu) na Tontan (Kahama) kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini ili wananchi waanze kupata huduma ya umeme na kwamba uzembe kwenye miradi hiyo haukubaliki.

Pia Dkt. Biteko amehamasisha utunzaji mazingira kwa kutumia nishati safi ya gesi inayotiliwa mkazo na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia ugawaji wa majiko ya gesi kwa wananchi.

Akitoa taarifa kuhusu mradi wa Kuzalisha Umeme Jua MWp 150, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Mhandisi Costa Lubagumya amesema utekelezaji wa mradi huo umekusudia kuongeza uzalishaji wa umeme kwa kutumia nishati mbadala ya jua na kuhakikisha umeme wa kutosha unapatikana katika Gridi ya Taifa ikiwemo mkoa wa Shinyanga na mikoa ya jirani ya Tabora, Mwanza na Mara na kuleta chachu ya maendeleo.
"Mradi huu unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza inahusisha ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua cha ukubwa wa Megawati 50 kikiwa na mashine umba moja yenye uwezo wa 1x40MVA. Awamu ya pili itahusisha ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua cha Megawati 100 kikiwa na mashine umba mbili zenye uwezo wa 2x40MVA",ameeleza Mhandisi Lubagumya.

Amesema fedha iliyotengwa kutekelezwa kwa awamu ya kwanza ya mradi ni shilingi za kitanzania Bilioni 118.677 na fedha iliyopangwa kutekelezwa kwa awamu ya pili ya mradi ni shilingi Bilioni 204.419 na kufanya jumla kuwa shilingi Bilioni 323.096 ambapo kati ya hizo shilingi Bilioni 320.255 ni Mkopo kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) na shilingi Bilioni 2.841 ni fedha kutoka serikali ya Tanzania kama malipo ya fidia kwa wananchi waliotoa maeneo yao kupisha mradi.

"Awamu ya kwanza ya mradi inatekelezwa na Mkandarasi ambaye ni Kampuni ya Sinohydro Corporation Limited kutoka China ambapo mkataba wa ujenzi ulianza Desemba 8,2023 na unatarajiwa kukamilika Januari 2025. Kazi zinazoendelea hivi sasa ni pamoja na usanifu wa mradi na usafishaji wa eneo la mradi. Mradi huu una mshauri muelekezi ambaye ni muunganiko (Consortium) ya ARTELIA kutoka Ufaransa na ENEGIOVERDA kutoka Tanzania",ameongeza Mhandisi Lubagumya.

Amefafanua kuwa awamu ya pili ya mradi inatarajiwa kuanza mwezi Agosti 2024 na inategemewa kuchukua takribani miezi 12 kukamilika kwani baadhi ya kazi zitakuwa zimeshafanyika kwenye awamu ya kwanza.
"Katika kipindi hiki cha uongozi wa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, sekta ya uzalishaji umeme, usafirishaji na usambazaji zimeendelea kuimarika na kukua kwa kasi. TANESCO inatambua jukumu kubwa ililonalo la kuhakikisha nchi inatimiza azma ya kujenga uchumi wa taifa ambao unachochewa na upatikanaji umeme wa kutosha na wa uhakika ili kuvutia uwekezaji mkubwa wa viwanda na biashara",ameeleza Mhandisi Lubagumya.

Naye Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), bi. Celine Robert amesema utekelezaji wa mradi huo unatokana na ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Ufaransa ambapo katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi yanayoathiri upatikanaji wa huduma ya uhakika ya umeme ndiyo maana wameanzisha ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme jua ili wananchi wapate umeme wa uhakika.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo amewashukuru wakazi wa kata ya Talaga kwa kuupokea mradi huo na kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi anayetekeleza mradi huo ambaye pia amekuwa na ushirikiano mzuri kwa wananchi wa Kishapu.

"Tunawapongeza wananchi kwa kupokea mradi huu, tutaulinda mradi huu mkubwa ambao utanufaisha wananchi wa Kishapu - Shinyanga na taifa kwa ujumla. Ombi letu kubwa ni kwamba wananchi wa eneo hili wapewe ajira kwenye mradi huu",ameongeza Mhe. Butondo.

Ameeleza kuwa mradi huo licha ya kuongeza kiwango cha umeme kwenye gridi ya Taifa na kuboresha hali ya umeme kwenye maeneo mbalimbali nchini, Halmashauri ya Kishapu itafaidika na ushuru wa huduma utakaolipwa kutokana na mradi kuwepo kwenye eneo hilo.

Mhe. Butondo ametumia fursa hiyo kufikisha kilio cha wananchi kuhusu umeme kutofika kwenye baadhi ya vijiji hali inayochangiwa na kusuasua kwa Mkandarasi SUMA JKT ambapo vijiji 28 kati ya 128 vilivyopo wilayani Kishapu bado havijapata huduma ya umeme lakini changamoto zingine ni upungufu wa magari kwa TANESCO Kishapu likiwemo gari la dharura na barabara mbovu ikiwemo barabara ya Kolandoto Kishapu mpaka Lalago inayotumiwa ma magari mbalimbali inayopaswa kujengwa kwa kiwango cha lami.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko (katikati) akiweka jiwe la msingi Mradi uzalishaji Umeme wa Jua Megawati 150 wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 323 unaotekelezwa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko (katikati) akiweka jiwe la msingi Mradi uzalishaji Umeme wa Jua Megawati 150 wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 323 unaotekelezwa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga 
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko akisoma maandishi baada ya kuweka jiwe la msingi Mradi uzalishaji Umeme wa Jua Megawati 150 wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 323 unaotekelezwa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga 
Mhandisi Emmanuel Anderson Meneja Mradi wa Umeme Jua (MW 50) - Kishapu Tanesco akimwelezea Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko  kuhusu mradi wa Umeme Jua
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko akizungumza baada ya kupata maelezo ya mradi wa kuzalisha umeme jua kutoka kwa Mhandisi Emmanuel Anderson Meneja Mradi wa Umeme Jua (MW 50) - Kishapu Tanesco 
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko akizungumza wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi mradi wa uzalishaji umeme jua Megawati 150 wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Machi 14,2024.
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko akizungumza wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi mradi wa uzalishaji umeme jua Megawati 150 wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga, kushoto ni wabunge wa Mkoa wa Shinyanga
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko akizungumza wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi mradi wa uzalishaji umeme jua Megawati 150 wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga
Naibu Waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko akizungumza wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi mradi wa uzalishaji umeme jua Megawati 150 wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko akizungumza wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi mradi wa uzalishaji umeme jua Megawati 150 wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko akizungumza wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi mradi wa uzalishaji umeme jua Megawati 150 wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko akizungumza wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi mradi wa uzalishaji umeme jua Megawati 150 wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko akizungumza wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi mradi wa uzalishaji umeme jua Megawati 150 wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko akizungumza wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi mradi wa uzalishaji umeme jua Megawati 150 wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko akiteta jambo na  Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), bi. Celine Robert wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi mradi wa uzalishaji umeme jua Megawati 150 wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Mhandisi Costa Lubagumya akitoa taarifa ya mradi  wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi mradi wa uzalishaji umeme jua Megawati 150 wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Mhandisi Costa Lubagumya akitoa taarifa ya mradi wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi mradi wa uzalishaji umeme jua Megawati 150 wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), bi. Celine Robert akizungumza wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi mradi wa uzalishaji umeme jua Megawati 150 wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), bi. Celine Robert akizungumza wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi mradi wa uzalishaji umeme jua Megawati 150 wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo akizungumza wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi mradi wa uzalishaji umeme jua Megawati 150 wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo akizungumza wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi mradi wa uzalishaji umeme jua Megawati 150 wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. Iddi Kassim akizungumza wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi mradi wa uzalishaji umeme jua Megawati 150 wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba (CHADEMA) akizungumza wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi mradi wa uzalishaji umeme jua Megawati 150 wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba akizungumza wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi mradi wa uzalishaji umeme jua Megawati 150 wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. Iddi Kassim (kushoto) akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba (kulia) wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi mradi wa uzalishaji umeme jua Megawati 150 wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Joseph Mkude ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu akizungumza wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi mradi wa uzalishaji umeme jua Megawati 150 wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa akizungumza wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi mradi wa uzalishaji umeme jua Megawati 150 wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga


Wananchi wakifuatilia hafla ya Uwekaji jiwe la msingi mradi wa uzalishaji umeme jua.

Picha zote na Kadama Malunde 1 blog



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments