JAMII YAHIMIZWA KUWEKEZA MWENYE MFUKO WA UTT

Na Christina Cosmas, Morogoro


JAMII imehimizwa kujiunga na Mfuko wa kuwekeza kijamii UTT ili kuvuna faida kubwa mwisho wa mwaka na kuona faida ya kujiwekea akiba inayokua.

Mhasibu na muongozaji wa biashara katika mashirika na makampuni binafsi nchini Vaileth Msemwa amesema hayo wakati akitoa elimu ya Biashara na uwekezaji kwa wajasiriamali na wadau wa biashara iliyoandaliwa na Taasisi ya vijana inayojihusisha na masuala ya kukuza uchumi (SUYOO) iliyopo mkoani hapa.


Msemwa alisema zipo namna nyingi za kujiwekea fedha ikiwemo kuwekeza kwenye mfumo huo wa UTT ambao humfanya mwenye hisa kukua kila anapowekeza kiasi kikubwa cha pes ana hivyo kuwa na mavno makubwa mara mwaka unapoisha.


Anasema pesa inahitaji kupewa thamani kwa kuihifadhi kwenye vyombo vya kifedha ikiwemo benki au kwenye kibubu bila kuiingiza kwenye matumizi mengine jambo litakalosaidia mmliki wa fedha hiyo kufikia hatua kubwa kimaendeleo hata kama uchumi wake ni mdogo.


Aidha Msemwa aliitaka jamii kutambua kuwa pesa inanafasi ya kumsikiliza mtu ambapo haiwezi kufanya chochote ambacho haijaambiwa kufanya ikiwemo kuingia kwenye matumizi yasiyo ya lazima na hivyo kumfanya mmiliki kufanya anachotaka kwa malengo.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa SUYOO Suka Jumanne ameishauri jamii kujenga tabia ya kuboresha biashara zao na kukuza vipato vyao sambamba na kuwa na usimamizi mzuri kifedha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post