MADHEHEBU MBALIMBALI YA DINI YAKUSANYIKA SHINYANGA KUMUOMBEA DUA NA SALA RAIS MSTAAFU HAYATI ALI HASSAN MWINYI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

WANANCHI kutoka Madhehebu Mbalimbali ya kidini mkoani Shinyanga, wamemuombea Dua na Sala Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili nchini Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi apumzike kwa Amani.

Maombi hayo yamefanyika leo Machi 4 kwenye Viwanja vya Sabasaba Manispaa ya Shinyanga huku Mgeni Rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme.
Akizungumza kwenye maombi hayo,  Mndeme kwanza amewashukuru wananchi wa Shinyanga kutoka Madhehebu mbalimbali kujitokeza kumuombea Rais Mstaafu Hayati Ali Hassan Mwinyi apumzike kwa Amani, na kuahidi kwamba watayaenzi yale mema ambayo amewaachia.

“Tumekusanyika hapa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kutoka Madhehebu mbalimbali ili tumombee Dua na Sala Rais wetu Mstaafu Hayati Ali Hassan Mwinyi ili Mwenyezi Mungu ampokee katika Ufalme wake na ampatie pumziko la Amani,”amesema Mndeme.
“Tumuombee pia Rais Wetu Samia Suluhu Hassan kwa Msiba huu Mzito ambao ameupata kwa kuondokewa na kiongozi Mkubwa ambaye alikuwa akimtegemea pia katika ushauri mbalimbali namna ya kuongoza nchi na kuwatumikia Watanzania,”ameongeza Mndeme.

Aidha, aliitakia pia pole Familia yote ya Marehemu Hayati Ali Hassan Mwinyi pamoja na Wajane ambao wameachwa kwamba Mwenyezi Mungu awapatie faraja katika kipindi hiki kigumu ambacho wameondokewa na mpendwa wao.
Katika hatua nyingine Mdeme, amewakaribisha Wananchi wa Shinyanga na viongozi mbalimbali, kwamba wafike kwenye Ofisi za Mkoa huo Kusaini Kitabu cha Maombolezo

Naye Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya, akizungumza kwenye Maombi hayo, amesema katika Mkoa huo hawatamsahau Rais Mwinyi kwa kutatua mgogoro mkubwa ambao ulikuwepo wa kiimani, ambapo aliutatua na kudumisha amani.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili nchini Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi alifariki dunia Februari 29 mwaka huu akiwa na miaka 98 alipokuwa akipatiwa Matibabu katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam na amezikwa Machi 2, 2024 huko Unguja, Zanzibar.

Alikuwa Rais wa Pili wa Tanzania kuanzia mwaka 1985 hadi 1995, Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe Amina.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiwa na viongozi wa dini kwenye Maombi ya kumuombea Dua na Sala Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi apumzike kwa Amani.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye, maombi ya kumuombea Dua na Sala Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi apumzike kwa Amani.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye maombi ya kumuombea Dua na Sala, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi apumzike kwa Amani.
Kiongozi wa dini ya Kikristo akiongoza Sala ya kumuombea Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi ampumzike kwa Amani.
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akiongoza Dua ya kumuombea Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Tanzania Ali Hassan Mwinyi apumzike kwa Amani.
Dua ya kumuombea Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Tanzania Ali Hassan Mwinyi ikiendelea.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Dua na Sala ya kumuombea Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi ampumzike kwa Amani.
Wanafunzi kutoka Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM)wakiwa kwenye Dua na Sala ya kumuombea Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi ampumzike kwa Amani.
Wananchi wa Shinyanga wakiwa kwenye Dua na Sala ya kumuombea Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi ampumzike kwa Amani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post