MKAYAISHI MAFUNDISHO YA MWENYEZI MUNGU ILI KUJIEPUSHA NA VITENDO VISIVYOFAA MTAKAPOREJEA NYUMBANI KUSUBIRI MATOKEO YENU - KANYEFU

 

Wanafunzi wa kidato cha sita wanaotarajia kuhitimu masomo yao ifikapo Mwezi Mei 2024 wametakiwa kuzingatia maadili na kuishi mafundisho ya Mwenyezi mungu ili kujiepusha na vitendo visivyofaa pindi watakaporejea nyumbani kusubiri matokeo.

Wito huo umetolewa na Mwanahabari na Mtangazaji wa Kituo cha matangazo Gold FM, Stephen Kanyefu  wakati alipomuwakilisha Mkurugenzi wa Kituo hicho Bi. Neema Mgheni leo Machi 23, 2024 katika Sherehe za Mahafali ya Kidato cha Sita tawi la UKWATA na Casfeta yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari Dakama illyopo Halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga.

Kanyefu amesema "Niwaombe wakati nahitimu elimu yenu ya kidato cha sita msisahau yale yote ambayo walimu wamewaelekeza kwa muda wote mlikuwa nao, wamewafundisha maadili wamewalekeza namna gani ya kuishi na jamii"

"Wazazi najua mko hapa mna furaha vijana wa kiume, wa kike leo wanakwenda kuhitimu mnapowapokea nyumbani muwakumbushe misingi ya maadili ambayo walimu wamewafundisha....Mafanikio yoyote ni nidhamu maadili"- amesema Kanyefu.

Aidha, akijibu risala iliyosomwa na Wanafunzi hao kwa niaba ya Bi. Ngheni, Kanyefu amesema GOLD FM ipo tayari kuwaunga mkono katika jitihada zao za kueneza injili kwani hatua hiyo itasaidia mafundisho hayo kuwafikia watu wengi zaidi jambo litakalochochea jamii kuishi katika hofu ya Mungu.

Awali wakisoma risala, Wahitimu hao waliomba kusaidiwa vifaa vya kuendeshea Ibaada, kama Bibilia agano la Kale na vitabu vya tenzi za rohoni, Ngoma na chombo cha sadaka, ambapo Bi. Neema Mghen ameahidi kuwapatia.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments