CHIEF CHARUMBIRA ACHAGULIWA TENA KUWA RAIS WA BUNGE LA AFRIKA 'PAP"

Mhe. Chifu Fortune Charumbira
***

Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP) leo Jumatatu Machi 25, 2024 limefanya uchaguzi mdogo  kujaza nafasi zilizo wazi ndani ya Ofisi  ambapo aliyekuwa Rais wa Bunge la Afrika PAP) Mhe. Chief Fortune Charumbira (Zimbabwe) amechaguliwa tena kuwa Rais wa Bunge la Afrika.

Katika uchaguzi huo pia Mhe. Prof. Massouda Mohamed Laghdaf (Mauritania) amechaguliwa tena kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika huku Mhe. Djidda Mamar Mahamat (Chad) akichaguliwa kuwa Makamu wa nne wa Rais wa Bunge la Afrika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments