KIGAHE AONGOZA UJUMBE WA TANZANI KATIKA MKUTANO WA  SCTIFI - EACNaibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Stephen Mbundi akiongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) kilichofanyika jijini Arusha tarehe 09 Februari 2024.

Mkutano huo ulijumuisha Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo DRC na Sudani kusini uliongozwa na Südani Kusini kama Mwenyekiti.

Ujumbe wa Tanzania ulijumuisha wajumbe kutoka Wizara ya Fedha, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara(TANTRADE), Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Tume ya Ushindani (FCC) na Mamlaka ya Mauzo ya Bidhaa Nje ya Nchi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post