KAMANDA MAGOMI AONGOZA ASKARI POLISI KUPANDA MITI SHINYANGA

 

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP Janeth Magomi akipanda mti.

Na Mwandisi wetu Malunde 1 Blog Shinyanga 

JESHI la Polisi mkoani Shinyanga, limepanda miti katika maeneo ya  Kambi na maeneo ya makazi ya Askari polisi wa  Jeshi hilo ili kuboresha mazingira pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Zoezi hilo la upandaji miti limefanyika leo Febuari 14, 2024 ambapo miti 1600 imepandwa katika maeneo ya kambi ya Jeshi la Polisi (FFU) na eneo la makazi ya Askari polisi uwanja wa polisi Kambarage .


Akizungumza wakati wa kupanda miti, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amesema Jeshi hilo linaunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kampeni ya upandaji miti ili kuboresha mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

“Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga tumepanda Miti 1600, lengo ni kuunga mkono juhudi za viongozi wetu katika kampeni ya upandaji miti kuboresha mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,”amesema Magomi.

“Katika kampeni ya upandaji miti tunataka Shinyanga iwe ya kijani, na miti ambayo tunaipanda tunataka ilindwe na ikue, ,”ameongeza Magomi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP Janeth Magomi akimwagilia mti wake baada ya kupanda mti
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP Janeth Magomi akipanda mti

Askari Polisi mkoa wa  Shinyanga wakionyesha utayari wa kupanda miti katika maeneo ya makazi yao
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP Janeth Magomi akimfundisha uzalendo mtoto juu ya utunzaji wa mazingira
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP Janeth Magomi akiongoza zoezi la upandaji miti
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP Janeth Magomi akimfundisha uzalendo mtoto juu ya utunzaji wa mazingira

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments