DKT. NCHIMBI AMJULIA HALI OLEMEIRUT HOSPITALINI PAMOJA NA KUMTEMBELEA KADA WA CCM PETER NIBOYE NYUMBANI KWAKE

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, leo Jumamosi Februari 3, 2024, amemtembelea na kumjulia hali Ndugu Loth Lazaro Olemeirut, Katibu wa CCM wa Wilaya ya Rorya, Mkoa wa Mara, ambaye amelazwa kwa ajili ya matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili – Mloganzila, jijini Dar Es Salaam. Kushoto ni Daktari Bingwa, Elineema Meda.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amemtembelea na kumjulia hali Ndugu Loth Lazaro Olemeirut, Katibu wa CCM wa Wilaya ya Rorya, mkoani Mara, leo Jumamosi, Februari 3, 2024, ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili – Mloganzila, jijini Dar Es Salaam, kwa ajili ya matibabu. Kushoto ni Daktari Bingwa, Elineema Meda.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amemtembelea na kumjulia hali Ndugu Peter Niboye, ambaye ni Kada wa CCM, anayeendelea ahueni akiwa nyumbani, jijini Dar Es Salaam, baada ya kutoka hospitali alikokuwa amelazwa hapo awali kwa ajili ya matibabu. Kushoto ni baba mzazi wa Peter, Mzee Josephat Niboye.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amemtembelea na kumjulia hali Ndugu Peter Niboye, ambaye ni Kada wa CCM, anayeendelea kupata ahueni akiwa nyumbani, jijini Dar Es Salaam, baada ya kutoka hospitali alikokuwa amelazwa hapo awali kwa ajili ya matibabu. Kushoto ni baba mzazi wa Peter, Mzee Josephat Niboye na kulia ni Bi. Edith Niboye, mama mzazi wa kada huyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments